Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo Alhamis kuwa watafanya hivyo pindi watakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa.
Taarifa hiyo ya Ummy imekuja muda mfupi baada ya Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu akusema kwamba madaktari wa Kenya wamesema Lissu hawezi kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya kumpatiwa matibabu.
Mbunge Nyalandu ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Facebook na Twitter kwamba mipango ya kumsafirisha Lissu ambayo walikuwa wanafanya itasimama kwa sasa kutokana na ushauri wa madaktari hao ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa vinginevyo.
No comments:
Post a Comment