Thursday, August 24

Watumia akaunti binafsi kutapeli watalii

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Aloyce Nzuki 


Dodoma.Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Aloyce Nzuki amesema kuna ujanja unaotumiwa na baadhi ya watu  kwa kuwataka watalii kulipa fedha kwenye akaunti zao nje ya nchi.
Akifungua Warsha ya wadau wa kanda ya kati kwa ajili ya mapitio ya Sera mpya ya utalii, Dk Nzuki amesema taifa linapata hasara kutokana na ujanja huo.
Amesema  sasa kuna kila sababu ya baadhi ya idara kushirikiana kukomesha jambo hill.
"Utakuta TRA wanakuja kukagua nakueleza kiwango kilichopaswa kulipwa na watalii na kuonekana kuko chini kumbe kuna wajanja wanawasiliana na watalii huko na kuwaambia kiwango fulani  waingize kwenye akaunti zao nje kabla ya kuingia nchini," amesema Nzuki

No comments:

Post a Comment