Friday, October 20

Umoja wa Ulaya wakataa kuingilia suala la Catalonia

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekataa kusaidia kuutatua mgogoro wa jimbo la Catalonia wakisema ni wajibu wa serikali kuu ya mjini Madrid na Barcelona  kutafuta suluhu ya mkwamo huo wa kisiasa.

Belgien EU-Gipfel (Reuters/V. Mayo)
Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk aliwaeleza waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels  kuwa suala la Catalonia haliko katika ajenda za mkutano huo.
" Sisi sote tuna mawazo yetu, hisia  na tathimini zetu lakini kwa taarifa tu hakuna nafasi ya Umoja wa Ulaya kuingilia mgogoro huo na nchi wanachama wanaelewa fika kuwa hakuna nafasi hiyo".  Alisema Tusk.
Hayo yanajiri mnamo wakati rais wa jimbo la Catalonia  Carles Puigdemont akipuuza muda wa mwisho aliopewa na serikali ya mjini Madrid  kubatilisha nia  yake ya  kutaka kutangaza uhuru wa jimbo hilo ambapo siku tatu alizopewa kufanya hivyo zimemalizika asubuhi ya leo na badala yake kiongozi huyo amemuandikia barua waziri mkuu Mariano Rajoy akitishia kutangaza uhuru wa jimbo la Catalonia.
"Puigdemont amesema " Iwapo serikali ya mjini Madrid itaendelea kukataa majadiliano pamoja na kuzima suala hili basi bunge la Catalonia litaendelea" alisema Puigdemont.
Rajoy anapanga kutumia ibara ya 155 ya katiba ya mwaka 1978 ambayo inamruhusu kuchukua mamlaka  ya jimbo lolote iwapo itabainika limevunja sheria.
Kakao maalumu cha baraza la mawaziri kimepangwa kufanyika Jumamosi ili kuandaa orodha ya hatua kwa ajili ya kuidhinishwa na seneti
Serikali ya Uhispania yapanga kumpokonya madaraka Puigdemont
Spanien Carles Puigdemont Premier der Regionalregierung (Reuters/A. Gea)
Kiongozi wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont
Hatua zinazofikiriwa ni pamoja na kumuondolea madaraka ya urais kiongozi wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont, kulipokonya jimbo hilo madaraka ya kusimamia masuala ya elimu na shule, kuitisha uchaguzi mpya, kuvunja bunge la jimbo hilo pamoja na kudhibiti vyombo vya habari vya umma  vinavyoonekana kuwa njia inayotumiwa  na jimbo hilo kutangaza nia yake ya kutafuta uhuru wa jimbo hilo.
Hadi sasa Puigdemont ametoa mwito wa kufanyika majadiliano kati ya uongozi wa jimbo hilo na serikali ya mjini Madrid pamoja na wapatanishi wa kimataifa.
Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akizungumzia suala hilo mjini Brussels amesema kuwa wanaunga mkono msimamo wa serikali ya Uhispania  na kuongeza kuwa ana mataumaini suluhu itapatikana kwa kuzingatia katiba  ya Uhispania huku Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte akisema  hilo ni suala la ndani kauli iliyoungwa mkono na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyefanya kikao cha faragha na  na Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy pembezoni mwa mktano huo wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.
Spanien Mariano Rajoy im Parlament (Reuters/J. Medina)
Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia wa Ufaransa aliezungumza na shirika la habari la Reuters Macron  alisema ana imani kubwa na Rajoy katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa kisiasa.  Naye Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mgogoro wa Catalonia ni suala la ndani la Uhispania na kukosoa undumilakuwili wa nchi za magharibi kwa kuunga mkono suala la Kosovo na kujiweka kando katika masuala mengine  kama hayo.
Wakazi wa Catalonia wapatao milioni 7.5 wamegawanyika kuhusiana na hoja hiyo ya kujitenga  ambapo wapiga kura wengi wanaopinga uhuru wa wa jimbo hilo walijiweka kando na kura hiyo ya maoni ambayo ilitangazwa kuwa ni batili na mahakama ya kikatiba ya Uhispania.
Wakati huohuo viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujaribu kutafuta njia za kuharakisha mazungumzo yanayohusiana na mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo ujulikanao kama Brexit. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hana mashaka yoyote   na anaimani Umoja wa Ulaya na Uingereza watapata mafanikio katika suala hilo la Brexit.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema mazingira yanayowekwa na viongozi hao wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na suala hilo yatasaidia kuwezesha kusonga mbele kwa mchakato huo wa Brexit.

Tillerson ajaribu tena kusuluhisha mgogoro wa Ghuba

Marekani itajaribu tena kuutatua mgogoro kati ya Qatar na Saudi arabia uliouchochea, wakati Waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson akielekea katika eneo hilo. Hata hivyo hana matumaini ya kuwepo mafanikio.

Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, Rex Tillerson (Reuters/Y. Gripas)
Mjumbe huyo mkuu katika serikali ya Donald Trump anatarajiwa kuondoka Marekani mwishoni mwa juma hili kuelekea Saudi Arabia na pia Qatar kwa mazungumzo juu ya kile kinachotajwa kama kuvunjika kwa mahusiano ya nchi hizo mbili. Tillerson amesema baadhi ya pande husika zinaonekana kusita kuingia katika mazungumzo.
"Sina matarajio makubwa ya mafanikio kupatikana hivi karibuni," alikiri Tillerson  hapo jana alhamisi katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la Bloomberg. Rex Tillerson aliyewahi kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya nishati ya ExxonMobil, analielewa vyema eneo la Ghuba kutokana na uzoefu wake wa kujadili na viongozi wa kifalme wa nchi hiyo, juu ya mikataba au mipango ya mafuta na gesi.
Trump, aliyezidi kuchochoea mgogoro huo kwa kuungana na Saudi Arabia  na kuishutumu Qatar kwa kuunga mkono ugaidi, ametabiri kwamba mgogoro utasuluhishwa. Lakini mgogoro huu wa hivi karibuni wa kidiplomasia ni wa kukanganya, wakati washirika wa marekani wakitupiana lawama hata wakati Marekani ikijaribu  kushughulikia Iran na masuala ya ghasia zinazotokana na ugaidi.
Iran yafaidika na mzozo?
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Bahrain (Picture alliance/abaca/Stringer)
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Bahrain
Saudi Arabia, Bahrain, Umoja wa falme  za kiarabu na Misri zilivunja mahusiano ya kidiplomasia na Qatar mwzi Juni mwaka huu ikiishutumu kwa kuunga mkono ugaidi na kujipendekeza kwa Iran. Pande hizo  zimekuwa zikizozana kuanzia wakati huo licha ya juhudi kutoka Kuwait, na ziara ambayo haikuwa ya mafanikio ya Tillerson mwezi Julai mwaka huu, kujaribu kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya kusuluhisha mgogoro.
Kundi hilo limekuwa  na nguvu katika uchumi wa Qatar iliyo tajiri kwa mafuta na kusababisha mvutano mpya katika eneo linaloyumba la Mashariki ya Kati, Uturuki ikijiunga na Qatar na Misri nayo ikionyesha uungaji mkono wake katika eneo la ghuba.
Wakati huo huo, Iran ambayo ni hasimu  wa Marekani huenda  ikafaidika kutoklana na  mfawanyiko huo katika kambi  hiyo ya mataifa yanayounga mkono nchi za magharibi na viongozi wa kijeshi  wa Marekani wana wasiwasi kuhusua athari zake za muda mrefu. Baada ya Trump kuunga mkono juhudi za kuitenga qatar licha ya kuwa mshirika wa kijeshi wa Marekani na  Marekani kuwa na  kituo cha kijeshi nchini humo,  badom kiongozi huyo wa Marekani hakutoa wito wa mazungumzo ya  kutafuta suluhisho.

UN yatoa Dola160 milioni nchini



Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez 
Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200 milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali Kigoma.
Nusu ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.
Oktoba 24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500 wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’
Akizungumzia maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.

Necta yaweka hadharani matokeo darasa la saba

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Chares Msonde 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba leo Oktoba 20,2017.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.
Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .
Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.
Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.
Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.
"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.
"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.
Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine  (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas  (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).
Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).
Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.
Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara.

Ajali ya Hiace, lori yasababisha vifo vya watu watano

Muleba. Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.
Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.
Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.
Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.

Obama na Bush wakosoa uongozi wa Trump

Marais wa zamani Barrack Obama na George BushHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES/REUTERS
Image captionMarais wa zamani Barrack Obama na George Bush
Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.
Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.
Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.
Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.
Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.
Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.
lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.
Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.
Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

Korea Kaskazini yaionya Australia kutoshirikiana na Marekani

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UnHaki miliki ya pichaKOREAN CENTRAL NEWS AGENCY
Image captionRais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilimwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.
''Wametuma barua hizi kwa mataifa mengi , kama barua iliosambazwa'', alisema Bwana Turnbull kwa kituo kimoja cha redio 3AW.
Waziri wa maswala ya kigeni Julie Bishop aliitaja barua hiyo kuwa hatua isiokuwa ya kawaida ya Korea Kaskazini.
Raia wa marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull
Image captionRaia wa marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull
Baadaye bwana Turnbull alionekana kutojali umuhimu wake akiifananisha na ufyozi na malalamishi kuhusu Donald Trump unaotolewa na Korea Kaskazini.
Hatahivyo wote wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya taifa hilo zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliana ya kimataifa.
Siku ya Jumamosi Pyonyang iliionya Australia kwamba haitaweza kuzuia janga iwapo itashirikiana na sera za Marekani dhidi ya utawala wa Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kupitia kufanyia majaribio kombora lake la kinyuklia mbali na kurusha makombora mawili juu ya anga ya taifa la Japan.
Marekani imejibu kwa vitisho vya kijeshi , lakini waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasisitiza kuwa bwana Trump yuko tayari kuutatua mgogoro huo kupitia diplomasia.

Afisa mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya Ezra Chiloba ajiondoa

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi ya IEBC Ezra ChilobaHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionAfisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi ya IEBC Ezra Chiloba
Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.
Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo.
Kulingana na gazeti hilo afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.
Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria.
Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga
Image captionRais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga
Kulingana na Daily Nation Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafisa waliotajwa baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali kung'atuka.
Mahakama ya juu ilisema kuwa haikupata ushahidi kuhusu makosa yaliofanywa na maafisa lakini wanasiasa wamelalamika na kuishutumu tume hiyo kwa kujaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo mbali na wizi wa kura.
Uamuzi huo wa kuchukua likizo ulijadiliwa na mwenyekiti na bwana Chiloba anaamini kwamba kutokuwepo kwake hakutaathiri maandalizi ya tume hiyo kusimamia uchaguzi ulio huru na haki .

Uchafuzi ndio chanzo cha asilimia 16 ya vifo duniani

Uchafuzi ndio chanzo cha asilimia 16 ya vifo dunianiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchafuzi ndio chanzo cha asilimia 16 ya vifo duniani
Utafiti wa kimataifa uliofanywa umekadiria kwamba uchafu ndio chanzo cha vifo vya watu milioni tisa duniani kote katika kipindi cha mwaka 2015.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Lancet umechanganua taarifa za dunia kuhusiana na magonjwa yaliyosababishwa na uchafu wa mazingira kama vile magonjwa ya moyo na magonjwa ya kupooza.
Vifo hivyo vya mapema vinaelezwa kuweka asilimia 16 ya vifo duniani kote.
Uchafuzi wa anga ndio sababu kubwa, ikifuatiwa na uchafuzi wa maji.
Utafiti huo unaonesha kuwa karibu asilimia kubwa ya vifo hivyo vinavyotokana na uchafuzi vimetokea katika nchi zenye kipato cha chini na kati.

Kwa Picha: Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Kenya

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza wananchi kuadhimisha Sikukuu ya Mashujaa ambayo huadhimishwa kila 20 Oktoba.
Sikukuu hiyo hutumiwa kuwakumbuka na kuwatambua mashujaa waliopigania uhuru pamoja na Wakenya wengine waliotoa mchango wa kipekee kwa taifa baada ya uhuru.
Maadhimisho ya Mashujaa
Rais Kenyatta baada ya kuwasili uwanja wa Uhuru Park, Nairobi.
Kenyatta
Wananchi walipekuliwa na vikosi mbalimbali vya usalama vikisaidiwa na vijana wa huduma kwa taifa kabla ya kuingia uwanjani.
Usalama
Mkuu wa Majeshi Samson Mwathethe (kulia) hapa anaonekana akisalimiana na waziri wa mambo ya nje Amina Mohamed.
Mwathethe
Mwanasheria Mkuu Prof Githu Muigai akiingia uwanjani, kofia kichwani na macho yake akiyaelekeza kwa kamera...
Muigai
Mwanamume huyu alionekana kujiandaa kuliombea taifa, mkono wa kulia anaonekana kuinua Biblia na kushoto simu yake. Rais Kenyatta ametangaza Jumapili kuwa siku ya maombi ya taifa kuiombea nchi hiyo kabla ya uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika Alhamisi.
Mwumini
Waliohudhuria walitumia siku zao kujiwekea kumbukumbu.
Piga picha
Jeshi
Hawa ni askari wa magereza.
Askari wa magereza
Kulikuwa pia na burudani.
Bendi
Jeshi
Mwanajeshi
Kikosi cha polisi kilikuwa kimewakilishwa ilivyo...
Mbwa

Daktari aeleza hali ilivyokuwa alipokwenda kumtibu Kanumba


Dar es Salaam. Daktari Paplas Kagaiya aliyekuwa akimtibu msanii maarufu wa fani ya uigizaji filamu nchini, Steven Kanumba ametoa ushahidi Mahakama Kuu akieleza hali aliyoikuta alipokwenda nyumbani kwa msanii huyo.
Mbali na Dk Kagaiya, askari Polisi aliyemtia mbaroni msanii wa kike Elizabeth Michael, maarufu Lulu, pia ametoa ushahidi mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 20,2017.
Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kosa analodaiwa kulitenda  Aprili 7,2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Kanumba.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi kutoa ushahidi, Dk Kagaiya amesema alipofika nyumbani kwa Kanumba alikuta akiwa ameanguka na alimpima kiwango cha sukari na shinikizo la damu.
Amesema kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo, hivyo alishauri Kanumba apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dk Kagaiya amesema daktari katika kitengo cha dharura Muhimbili alipompima Kanumba aliwaeleza alikuwa tayari ameshafariki dunia.
Baada ya kupewa maelezo hayo, amesema walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Selander Bridge.
Shahidi huyo alipoulizwa na wakili wa Lulu, Peter Kibatala kama kuna vitu vyovyote alivyoviona eneo la tukio chumbani kwa Kanumba, ikiwemo chupa ya pombe alisema hakutambua chochote.
Katika hatua nyingine, askari Ester Zefania kutoka Kituo cha Polisi Msimbazi akitoa ushahidi amesema alikwenda kumkamata Lulu alfajiri, eneo la Bamaga kwa msaada wa Dk Kagaiya, ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa simu.
Akijibu swali la wakili Kibatala kama alimpeleka Lulu hospitalini kwa matibabu, shahidi huyo amesema ni kweli alimpeleka hospitali.
Hata hivyo, Zefania amesema Lulu hakumueleza kuwa alipigwa na Kanumba na wala hakuona majeraha. Alijibu hayo baada ya kuulizwa swali na wakili Kibatala.
Zefania amesema aliagizwa na mkuu wake wa kazi ampeleke Lulu hospitalini lakini hakujua alikuwa ana matatizo gani.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika itaendelea Jumatatu Oktoba 23,2017 kwa upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi wake.

Sauti ya Lissu yamliza Mkuu wa KKKT


Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesimulia alivyobubujikwa machozi baada ya kusikia sauti ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.
Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, amesema hayo baada ya Jumatano Oktoba 18,2017 Lissu kutoa salamu akiwashukuru Watanzania kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7,2017 mjini Dodoma.
Sauti ya Lissu katika video hiyo ilikuwa ni ya kwanza kusikika tangu apelekwe jijini Nairobi Septemba 7.  Alisikika akiwashukuru madaktari wa Nairobi na Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa kuokoa maisha yake.
Pia, amewashukuru viongozi wa dini na wananchi kwa kumuombea, na taasisi za kitaaluma  ndani na nje ya nchi ikiwemo TLS ambazo zilionyesha mshikamano mkubwa.
Akizungumza na Mwananchi, Askofu Shoo amesema alijikuta akitokwa machozi aliposikia sauti ya Lissu, akisema kupona kwake ni onyo kwa wale waliohusika.
 “Ninazidi kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyomuokoa na anavyozidi kumpa uponyaji. Kupona kwa Lissu ni jibu la Mungu na onyo kwa wale wote waliohusika. Mungu amesema hapana,” amesema.
Askofu Shoo amesema, “Mwenye masikio na asikie. Uhai wa mwanadamu ni kitu cha kuheshimu. Tusijaribiwe kujichukulia madaraka ya kuondoa uhai wa mtu hata kama uwezo tunao kwa maana Mungu hataki na wala hataacha kumwadhibu yeye aondoaye uhai wa ndugu yake kwa hiana.”