Saturday, September 30

CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO


Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 
SERIKALI ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 29.4 kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu ya ufundi stadi, utalii wa kijiolojia na kukarabati wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong. 
Bw. Doto James alisema kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 22.4 cha msaada huo kitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera, ambacho kitakapo kamilika kitadahili zaidi ya wanafunzi 400. 
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” alisema Bw. James 
Alieleza kuwa kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. 
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” alisema Bw. James 
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James alibainisha kuwa katika makubaliano ya msaada huo, Jamhuri ya watu wa China, itatoa kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Dar es Salaam. 
“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Alifafanua Bw. James 
Bw. Doto James alisema kuwa kiasi kingine cha shilingi  milioni 300 kitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha. 
Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa 
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo” aliongeza Bw. Doto James. 
Aliishukuru China kwa ushirikiano wake wa dhati na Tanzania tangu miaka ya 1960 na kwamba mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuipiga jeki Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong, amesema kuwa nchi yake inatarajia kwamba ujenzi wa Chuo Cha Ufundi VETA huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa. 
Kuhusu masauala ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea. 
“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii elfu 20 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” aliongeza Mhe. Haodong 
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo alisema kuwa hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.77 na kukuza ajira nchini. 
Ameitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyowekezwa kuwa ni pamoja na mradi wa miundombinu ya mtandao (Tanzania ICT Broadband backbone), Bomba la gesi la kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi wa kuboresha miundombinu ya Bandari, barabara na madaraja. 
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, ambaye alisema kuwa msaada wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA mkoani Kagera kitaongeza watalaamu watakaosaidia kuendeleza sekta ya viwanda nchini.

KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM ATEMBELEA VITUO VYA DALADALA


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akitoa maelekezo kwa afande Doria 72 Sgt John wa doria 26 alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. Afande Haji alielekeza wakamate magari yote yanayodaiwa.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es salaam (ZTO) Kamishna Msaidizi wa Polizi ACP Awadhi Haji akiongea na baadhi ya madereva wa Daladala ambao magari yao yalikamatwa kwa kutokulipa madeni alipotembelea kituo cha Daladala kilichopo Gerezani jijini Dar es salaam. 

Samaki wanao kanda miguu katika bwawa la Chemka Tanzania

Wengi tunapenda kufanyiwa massage au kukandwakandwa mwili, lakini umewahi kuwaza kuwa mkandaji anaweza kuwa Samaki? Inashangaza au siyo?
David Nkya anatupeleka mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania kwenye Bwawa liiitwalo Chemka, humo kuna Samaki wanawafanyia watu Massage.

Mwanablogu atozwa faini kwa kudanganya aliponya saratani bila kutumia dawa

Belle GibsonHaki miliki ya picha9 NEWS / 60 MINUTES
Image captionBelle Gibson alidanganya kuwa dawa za kiasili zilimzaidia kuponya saratani
Mwandishi mmoja ambaye huchapisha makala yake kwenye mitandao ya kijamii ametozwa faini ya dola elfu 410 kwa kuwapotosha wafuasi wake.
Belle Gibson, mwenye umri wa miaka 25 alipata umaarufu nchini Australia baada ya kudai kuwa aliweza kuponya saratani ya ubongo kupitia chakula tu na bila kutumia dawa yoyote.
Alitengeneza programu tumishi na kitabu cha upishi ambacho kilipokelewa vizuri sana lakini baadaye alikiri kuwa hakuwa anaugua saratani.
Jaji aliyesikiza kesi yake alisema kuwa kuna watu ambao waliamini na kutenda vile alivyoandika na kusema Gibson.
Gibson alikuwa maarufiu sana kwenye mitandao ya kijamii kupitia madai yake kuwa ameweza kuponya saratani kwa kutumia dawa za kiasili, na kususia vyakula vyenye sukari.
Jaji Debbie Mortimer alisema kuwa makala yake Gibson yalifuatwa sana na makundi yanayozingatiwa kuwa dhaifu; wasichana wadogo, wanaotafuta hifadhi, watoto wagonjwa
Programu tumishi na kitabu chake Gibson ambavyo vyote villitwa 'The Whole Pantry' vilimwezesha kupata dola elfu 420 za Australia na alikuwa ameahidi kutoa asilimia yake kama msaada kwa wasiojiweza, lakini hakufanya hivyo.

Roketi kuanza kusafirisha watu kati ya miji kwa dakika tu

roketiHaki miliki ya pichaSPACEX
Image captionItachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Hivi karibuni watu wataweza kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kutumia roketi, safari ambayo itachukua dakika chache tu, kulingana na mjasiriamali Elon Musk.
Musk aliahidi haya katika kongamano moja nchini Australia.
Inasemekana kuwa itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Musk amesema pia kuwa mwaka wa 2024, ataanza kuwasafirisha watu hadi Mars. Kampuni yake ya SpaceX itaanza kujenga meli za kipekee zitakazofanikisha haya, mwaka ujao.
Kwa sasa kampuni yake inatengeneza ain amoja tu ya roketi; aina ya BFR ambayo inaweza kufanya kazi tofauti tofauti ikiwemo kupeleka watu kwenye mwezi na Mars.
"Safari ambazo watu wengi wanaona kuwa ndefu zinaweza kukamilika kwa chini ya nusu-saa," aliambia umati wa watu mjini Adelaide.
"Baadhi ya wateja wetu wanataka kuona BFR ikiruka mara kadhaa kabla yaya kuwa na imani nayo," Musk alisema.
"Kwa hivyo tunachotaka kufanya ni kujenga roketi kadhaa aina ya Falcon 9 na Dragon, ili wateja wawe na urahisi, na ikiwa wanataka kutumia roketi za kale, bado tuna kadhaa."
Musk, alianza mipango ya kufanikisha safari za Mars mwaka wa 2016, na amerejea na habari zaidi.
Musk amevutia watu wengi sana ambao wamependezwa na miradi yake. Na ingawa ahadi zake mara nyingi zimechukua muda mrefu kutekeleza, baadhi imetimia.
Hii ni pamoja na kutuma na kurejesha roketi 16 duniani baada ya roketi hizo kumaliza misheni yao. Roketi mbili kati ya hizo 16 zimeweza kusafiri tena mara ya pili.
Anasema cha muhimu sana kwake ni kuunda rtoiketi ambazo zinawza kutumika tena na tena kama ndege, kwani ni inagharimu pesa nyingi sana kutengeneza roketi.

Mwanamke ajioa nchini Italia

Laura Mesi, who married herself, cuts her wedding cakeHaki miliki ya pichaMICAELA MARTINI
Image captionFuraha yangu haitegemei uwepo wa mwanamume
Mwanamke moja nchini Italia amejioa yeye mwenyewe kwenye sherehe iliyokuwa na vazi kamili la harusi, keki na wageni 70.
"Ninaamini kuwa kila mmoja wetu ni lazima ajipende," alisema Luara Mesi mwenye miaka 40
Wanaounga mkono ndoa kama hizo wanasema kuwa suala kuu ni kujipenda.
Laura anasema kuwa suala la kujioa lilimkujia miaka miwili iliyopita, baada ya miak 12 ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Laura Mesi and her bridesmaidsHaki miliki ya pichaMICAELA MARTINI
Image captionNdoa ya Bi Mesi
"Niliwaambia marafiki zangu na familia kuwa sijapata mpenzi na nikiwa na umri wa miaka 40 nitajioa." aliliambia gazeti la La Repubblica.
"Ikiwa siku moja nitapata mwanamume ambaye nitapanga kuishi naye nitafurahi, lakini furaha yangu haimtegemei yeye."
Bi Mesi anasema kuwa yeye ndiye mwanamke wa Kwanza nchini Italia kufanya harusi ya mtu mmoja.
Carved watermelon at the solo wedding of Laura MesiHaki miliki ya pichaMICAELA MARTINI
Image captionTunda la kusherehekea ndoa ya Laura Mesi
Kati ya maoni yaliyowekwa kwenye picha za Bi Mesi ni pamoja na , "vibaya sana", "umechanganyikiwa" na "kuna tatizo na ubongo wako."
Hata hivyo Bi Mesi ametupilia mbali maoni hayo akisema hakuna mtu atazima tabasamu lake.

Kufanya kazi ndogo ndogo ya nyumbani kunaweza kuboresha maisha ya wazee.

mnunuzi na bidhaaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kubeba bidhaa waliyonunua, kufanya ukulima kidogo kwenye bustani na kusafisha nyumba kunaweza kuwasaidia watu wazee kuwa na maisha marefu yenye afya, kulingana na wataalamu wa afya.
Madaktari wanasema kuwa mamilioni ya watu wazee huanguka kila mara kwa sababu hawafanyi mazoezi.
Robo ya watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65 hawafanyi mazoezi yoyote ya kuwapa nguvu, kulingana na madaktari ambao wanaonya kuwa kuongezeka kwa nafasi za kunua bidha mitandaoni kunamaanisha kuwa watu hawaendi madukani na kubeba bidhaa kutoka huko hadi nyumbani kwao.
Madaktari wanasema kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu wanapoendelea kuongeza miaka.
Ni vyema kwa watu kufanya mazoezi ya kuwapa nguvu angalau mara mbili kwa wiki, kama kubeba mizigo mizito. Lakini utafiti uliohusisha zaidi ya watu wakongwe elfu mbili nchini Uingereza ulionyesha kuwa wengi wao hawafanyi mazoezi kamwe.
Mmoja kati ya watu watano alisema hawajui kufanya mazoezi na wengine walisema hawataki tu kuyafanya.
Ajali za kuanguka miongoni mwa watu wazee huchangia asilimia kubwa ya majeraha inayohusisha kuvunjika kwa mifupa ya sehemu ya kiuno, na hugharimu takriban dola bilioni moja kutibu kila mwaka.
Profesa Karen Middleton, ni afisa mkuu mtendaji wa CSP, na anasema tunakuwa dhaifu tunapokuwa wazee.
"Utafiti unaonyesha kuwa kufanya mazoezi ya kutupa nguvu kuna faida nyingi na ni muhimu watu kuzingatia haya."
Anasema inaweza kuwa kupalilia shambani au kusimama mara 10 kutoka kwenye kiti.
"Siku hizi tunabeba mifuko chache sana tukitoka dukani na mara nyingi tunanunua bidhaa mitandaaoni."
Profesa Middleton anasema kubeba mifuko ya chakula na bidhaa nyingine kutoka sokoni kunachangia mazooezi kwenye misuli.

Punda amezea mate gari lenye rangi ya karoti

Gari la McClaren Spider na pundaHaki miliki ya pichaMCCLAREN/ISTOCK
Image captionJe ni njaa iliyom'bana punda Vitus?
Mahakama ya Ujerumani Alhamisi itaamua Alhamisi iwapo mmiliki wa punda aliyejaribu kulitafuna gari anapswa kulipia gharama za uharibifu wa gari hilo.
Mnamo Septemba 15 mwaka jana, Markus Zahn aliliegesha gari lake kwenye eneo linalopakana na uwanja alikowekwa punda huko Vogelsberg, wiliya iliopo kwenye jimb la Hesse Ujerumani.
Punda kwa jina Vitus aliitafuna sehemu ya nyuma ya gari hilo, anasema.
Polisi wanaeleza huenda Vitus alidhani gari hilo ni karoti.
Farasi na punda katika uchaguzi wa urais Kenya
Lakini mmiliki wa punda huyo anapinga tuhuma hizo na badala yake anaitisha €6,000 kulipia gharama za uharibifu.
Anasema huenda Vitus hakufanya hilo na kwamba bwana Zahn hange egesha gari lake linalodiawa kuwa na thamani ya Euro 300,000 - karibu na uwanja huo.
Mahakama ya kiraia ya Giessen inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi iliyogubika vyombo vya habari kitaifa.

Unene wa mwili na umri mkubwa vinachangia wanawake kujifungua kupitia upasuaji

BabyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUnene wa mwili na umri mkubwa vinachangia wanawake kujifungua kwa upasuaji
Unene wa mwili kupita kiasi na mama wazee ndicho chanzo cha kuwepo maelfu ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji, kwa mujibu wa wataalamu.
Takwimu zinaonyesha kuwa upasuaji uliopangwa au wa dharura umeongezeka licha ya kushuka kwa idadi watoto wanaozaliwa kwa jumla.
Chuo cha Royal College of Obstetricians and Gynaecologists nchini Uingereza kinasema kwa kuongeza kwa matatizo wakati wa kujifungua kumechangiwa na unene kupita kiasi na umri mkubwa.
Zaidi ya robo ya watoto wanaozaliwa nchini Uingereza huzaliwa kwa njia ya upasuaji.
The Borrett familyHaki miliki ya pichaWWW.ZOEGIBBSPHOTOGRAPHY.CO.UK
Image captionUnene wa mwili na umri mkubwa vinachangia wanawake kujifungua kwa upasuaji
Mtoto huzaliwa kwa njia ya upasuaji wakati mama anakatwa tumbo lake.
Upasuaji huwa wa aina mbili.
Kwanza kuna upasuaji wa kupangwa, huu ni ule ambao hupangwa mapema hasa kutokana na sababu za kiafya sanasana wakati mtoto amelala upande usiotakikana au mtoto ni mkubwa zaidi.
Upasuaji wa pili ni ule wa dharura ambao mara nyingi hufanyika wakati kuna matatizo wakati wa kujifungua.
Alexandra Borrett with LucyHaki miliki ya pichaALEXANDRA BORRETT
Image captionUnene wa mwili na umri mkubwa vinachangia wanawake kujifungua kwa upasuaji

IS imetoa kanda ya sauti ya Abu Bakr al-Baghdadi.

BaghdadiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUrusi na Iran zimesema kiongozi huyo amekufa lakini Marekani imekataa
Wanamgambo wa Islamic State wametoa kile kinachoonekana kuwa ni kanda ya sauti ya kiongozi wa kundi hilo, Abu Bakr al-Baghdadi.
Mzungumzaji aliye na sauti kama ya kiongozi huyo wa IS anasikika akitaja tishio la hivi karibuni la Korea kaskazini dhidi ya Japan na Marekani.
Anazungumzia pia vita vya kupigania ngome za IS kama Mosul, mji uliodhibitiwa upya na vikosi vya Iraq mwezi Julai.
Baghdadi,ambaye anasakwa hajaonekana mbele ya umma tangu Julai 2014 jambo lililozusha uvumi mkubwa kuhusu hatma yake.
Mwisho alipoonekana alikuwa anatoa hotuba katika mskiti mkubwa wa al Nuri mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo na kulitangaza kuwa eneo wanalo litawala.
Aliopulizwa kuhusu kanda hiyo ya sauti, msemaji wa vikosi vya Marekani vinavyopigana na IS, Ryan Dillon, amesema "pasi kuwepo ushahidi wa kuthibitishwa wa kifo chake, tumeendelea kuamini kwamba yuko hai".
Msemaji wa idara ya ulinzi ameiambia BBC: "tunahafahamu kuhusu kanda hiyo ya sauti inayodaiwa kuwa ya Abu Bakr Al-Baghdadi na tunachukua hatua kuikagua.
Wakati hatuna sababu ya kuwa na shaka ya uhalisi wake, hatuwezi kuithibitisha kwa hivi sasa."
Kundi la wanamgambo wa kiislamu IS, lilitambulika kwa ghasia dhidi ya raia na wafungwa, limesukumwa nyuma Iraq na Syria mwaka huu.