Unene wa mwili kupita kiasi na mama wazee ndicho chanzo cha kuwepo maelfu ya wanawake wanaojifungua kwa njia ya upasuaji, kwa mujibu wa wataalamu.
Takwimu zinaonyesha kuwa upasuaji uliopangwa au wa dharura umeongezeka licha ya kushuka kwa idadi watoto wanaozaliwa kwa jumla.
Chuo cha Royal College of Obstetricians and Gynaecologists nchini Uingereza kinasema kwa kuongeza kwa matatizo wakati wa kujifungua kumechangiwa na unene kupita kiasi na umri mkubwa.
Zaidi ya robo ya watoto wanaozaliwa nchini Uingereza huzaliwa kwa njia ya upasuaji.
Mtoto huzaliwa kwa njia ya upasuaji wakati mama anakatwa tumbo lake.
Upasuaji huwa wa aina mbili.
Kwanza kuna upasuaji wa kupangwa, huu ni ule ambao hupangwa mapema hasa kutokana na sababu za kiafya sanasana wakati mtoto amelala upande usiotakikana au mtoto ni mkubwa zaidi.
Upasuaji wa pili ni ule wa dharura ambao mara nyingi hufanyika wakati kuna matatizo wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment