Mwandishi mmoja ambaye huchapisha makala yake kwenye mitandao ya kijamii ametozwa faini ya dola elfu 410 kwa kuwapotosha wafuasi wake.
Belle Gibson, mwenye umri wa miaka 25 alipata umaarufu nchini Australia baada ya kudai kuwa aliweza kuponya saratani ya ubongo kupitia chakula tu na bila kutumia dawa yoyote.
Alitengeneza programu tumishi na kitabu cha upishi ambacho kilipokelewa vizuri sana lakini baadaye alikiri kuwa hakuwa anaugua saratani.
Jaji aliyesikiza kesi yake alisema kuwa kuna watu ambao waliamini na kutenda vile alivyoandika na kusema Gibson.
Gibson alikuwa maarufiu sana kwenye mitandao ya kijamii kupitia madai yake kuwa ameweza kuponya saratani kwa kutumia dawa za kiasili, na kususia vyakula vyenye sukari.
Jaji Debbie Mortimer alisema kuwa makala yake Gibson yalifuatwa sana na makundi yanayozingatiwa kuwa dhaifu; wasichana wadogo, wanaotafuta hifadhi, watoto wagonjwa
Programu tumishi na kitabu chake Gibson ambavyo vyote villitwa 'The Whole Pantry' vilimwezesha kupata dola elfu 420 za Australia na alikuwa ameahidi kutoa asilimia yake kama msaada kwa wasiojiweza, lakini hakufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment