Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionWanajeshi wanaounga mkono serikali ya Syria, wamekuwa wakiendelea na vita katika juhudi za kuwafurusha waasi kutoka mji wa Douma
Serikali ya Syria na mshirika wake Urusi zimeishutumu Israel kwa shambulio baya katika uwanja wa ndege za kijeshi za Syria.
Shambulio hilo la Jumatatu liliulenga uwanja wa ndege za kivita wa Tiyas unaofahamika kwa umaarufu kama T4, karibu na mji wa Homs. Waangalizi wanasema watu 14 wameuawa.
Israel, ambayo awali iliwahi kuyelnga maeneo nchini Syria bado haijatoa tamko lolote. Awali Syria iliilaumu Marekani kwa shambulio hilo.
Tukio hilo limetekelezwa huku jamii ya kimataifa ikiendelea kulaani shambulio la kemikali ambalo lilitekelezwa katika mji wa Douma ambao unashikiliwa na waasi. Marekani na Ufaransa zimetishia kulipiza kisasi.
Rais wa Marekani Donald Trump alimweleza Rais wa Syria kama "nduli" Jumapili na kuonya kwamba yeye pamoja na washirika wake Iran na Urusi "watalipia sana".
Many dead, including women and children, in mindless CHEMICAL attack in Syria. Area of atrocity is in lockdown and encircled by Syrian Army, making it completely inaccessible to outside world. President Putin, Russia and Iran are responsible for backing Animal Assad. Big price...
Bw Trump na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron walitoa taarifa siku hiyo na kuapa "kuchukua hatua kali na ya pamoja" kuhusiana na shambulio hilo.
Lakini maafisa wa Marekani wamekanusha uwezekano kwamba Marekani ndiyo iliyotekeleza shambulio hilo.
"Kwa sasa, Wizara ya Ulinzi haitekelezi mashambulio yoyote ya angani Syria," Pentagon imesema kupitia taarifa.
"Hata hivyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia zinazoendelea za kuwawajibisha wote wanaotumia silaha za kemikali, nchini Syria na kwingineko, kuhakikisha wanaadhibiwa."
Haki miliki ya pichaEVNImage captionMtoto akitibiwa baada ya linaloaminika kuwa shambulio la kemikali eneo la Douma
SANA awali waliripoti shambulio hilo katika uwanja wa Tayfur kama "shambulio linalodhaniwa kutekelezwa na Marekani", lakini baadaye wakaacha kuitaja Marekani.
Aprili mwaka 2017, Marekani ilirusha makombora 59 aina ya Tomahawk katika uwanja wa ndege za kivita wa Shayrat nchini Syria baada ya shambulio la kemikali kutekelezwa katika mji wa Khan Sheikhoun uliokuwa unashikiliwa na waasi.
Israel ilitekeleza pia mashambulio mengine makubwa dhidi ya Syria mapema mwezi huu.
Nini kilitokea Douma?
Duru za kimatibabu zinasema watu wengi walifariki katika shambulio hilo la Douma, mlinalopatikana Ghouta Mashariki.
Video moja ambayo imekuwa ikisambaa ambayo ilirekodiwa na wahudumu wa kujitolea wafahamikao kama White Helmets linawaonesha maiti za wanaume, wanawake na watoto kadha ndani ya jumba moja, maiti nyingi zikiwa na povu mdomoni.
Hata hivyo, imekuwa vigumu kubaini hasa nini kilitokea na idadi kamili ya waliofariki.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWatoto wakifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu eneo la Douma
Syria na Urusi wote wamekana taarifa kwamba shambulio la kemikali lilitekelezwa, na wameafikiana mkataba wa kuwahamisha waasi ambao walikuwa wakishikilia mji wa Douma.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana Jumatatu kujadili mzozo huo.
Lakini sio tatizo linaloshuhudiwa kwa Wasomali tu. Vijana wanataja kukwama kupiga hatua ya kufunga ndoa kutokana na gharama hizo kubwa za mahari wanazoshindwa kuzimudu.
Mahari inavyotozwa katika baadhi ya nchi za Afrika:
Somalia:
Idadi ya ngamia au pesa taslimu mwanamume anazoahidi kumlipa mkewe kama mahari huitwa Meher.
Sio lazima Meher ilipwe moja kwa moja lakini huwa ni kama ahadi wameandikiwa, na mume hana budi kulipa katika kipindi cha ndoa.
Zamani ngamia ndio waliotumika kulipa mahari hayo lakini siku hizi mtindo umebadilika na pesa taslimu ndio zinazothaminiwa zaidi katika jamii hii.
Kijana anaweza kutakiwa kulipa hadi dola elfu kumi za Marekani kwa bibi harusi. Na kila thamani ya mahari inapokuwa kubwa ndio huonekana kuwa fahari kubwa kwa bibi harusi na familia yake na pia hudhihirisha ukubwa wa thamani ya mke anayeolewa.
Lakini tatizo kubwa ni kwamba vijana wengi hawawezi kugharimia mahari inayoitishwa na baadhi yao huishia kuwa na deni la maisha.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionThamani ya mahari inapokuwa kubwa ndio huonekana kuwa fahari kubwa kwa bibi harusi na familia yake
Tanzania:
Tanzania, ni nchi nyingine inayotajwa kushuhudia viwango vikubwa vya mahari katika baadhi ya jamii.
Huenda ndio moja ya sababu inayowafanya baadhi ya vijana kutooa kwa njia rasmi.
Vigezo ni vingi vinavyobaini kiwango cha mahari atkachotozwa kijana, mfano katika baadhi ya jamii - weupe wa msichana humaanisha mahari zaidi, lakini pia kiwango cha elimu cha msichana anyechumbiwa.
Kwa kukadiria kijana huitishwa ng'ombe au pesa zenye thamani ya kati ya shilingi milioni 5 hadi milioni 20 za Tanzania.
Uganda:
Utamaduni huu ni wa kawaida nchini Uganda, zaidi kwa jamii zilizopo katika maeneo ya mashinani, lakini pia hutolewa katika maeneo ya mijini.
Mahari nchini humu hufuata msingi ambao umekuwepo - kutoa kitu ili upewe mke.
Lakini sasa kuna mtindo kwa baadhi ya familia kuandikishana mikataba na bwana harusi kama ithibati ya kulipa mahari anayoitishwa.
Inaaminika kuwa iwapo mke amemtoroka mumewe baada ya kuteta na akarudi kwao, familia yake haina budi ila kurudisha mahari yote aliyolipiwa.
Mnamo 2010 mahakama nchini humo iliamua kuwa utoaji mahari ni halali, lakini majaji walipiga marufuku mtindo huo wa kurudishwa mahari wakati ndoa inapovunjika.
Je ni kweli gharama ya juu ya mahari inawazuia vijana kufunga ndoa Afrika Mashariki?
Kenya:
Katiba nchini Kenya haishurutishi ulipaji wa mahari, lakini ni jambo linalofahamika kuwa mahari hulipwa katika jamii tofuati nchini.
Baadhi ya jamii kwa mfano kwa wafugaji husisitiza mahari ya mifugo, huku kwa jamii nyingine mali, pesa taslimu na hata madini hupokewa kama mahari.
Huwepo hisia kwamba kuna malipo aliyotolewa mke kwenda kwa mume.
Haki miliki ya pichaAALTONEN JUMBAImage captionAnne na Wilson Mutura waliwafurahisha wengi baada ya kutumia Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi mwaka 2017
Afrika Kusini:
Mahari hapa huitwa "lobola", ambapo mwanamume hukabidhi ima mali au ng'ombe kwa familia ya mke au kwa mara nyingine vyote - kama ishara kwamba yuko tayari kumuoa.
Malipo ya lobola ni ishara ya uwajibikaji wa mwanamume kumhudumia mkewe na huonekana kama ishara muhimu na inayohitajika katika kuendeleza utamaduni, na sio kana kwamba amemnunua mwanamke.
Mahari ni nini?
Utamaduni wa kutoa mahari upo katika nchi nyingi ulimwenguni zikiwemo barani Asia, mashariki ya kati sehemu kadhaa za Afrika na pia katika baadhi ya visiwa vya pasifiki.
Kiwango kinachotolewa hutofautiana kuanzia zawadi ndogo tu za kuendeleza utamaduni huo hadi maelfu ya dola za Marekani kwa mfano kama inavyoshuhudiwa katika ndoa za baadhi ya jamii.
Tangu jadi, utoaji mahari umekuwa ni utamaduni unaoheshimiwa na kuenziwa pakubwa hata miongoni mwa jamii za watu waliosoma na kuishi maisha ya kisasa.
Kwa kawaida mahari huwa ni kama mkataba wa makubaliano kabla ya ndoa ambapo mali kama ng'ombe, ngamia, mbuzi au hata pesa taslimu hulipwa na bwana harusi kwa familia ya bibi harusi ili apewe mke.
Iwapo mume hatotimiza mahari iliyokubaliwa kwa muda uliotolewa, kuna jamii ambao humrudisha mke nyumbani mpaka mume akamilishe kulipa mahari.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Na kwa namna ambavyo mambo yamekuwa yakibadilika na gharama kuongezeka, baadhi ya wadadisi wanasema utamaduni huu wa kutoa mahari unageuzwa kuwa njia ya kujinufaisha na kujigamba kwa mali badala ya kuwa utamaduni wa kuonyesha upendo na shukrani.
Mchambuzi wa masuala ya kijamii kutoka Tanzania Betty Masanja anasema, "Suala zima limegeuzwa na kumfanya mwanamke kuwa chombo au bidhaa tu."
''Hali inazidi kuwa mbaya kutokana na kuwa, watu wana shida za kiuchumi, umaskini umekithiri hasa kwa familia ambazo hazikusoma."
Ndio maana unaona hata jamii zinawaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo ili mahari ilipwe kuitajirisha familia.
Lakini sio suala la kujitajirisha tu, Betty anasema kuna kutothaminiwa kwa mtoto wa kike ambapo wengi huozeshwa ili mali ipatikane kusaidia kumuelimisha mtoto wa kiume.
Ameeleza: ''suala zima limegeuzwa na kumfanya mwanamke kuwa chombo au bidhaa tu''.
Haki miliki ya pichaPAImage captionMshindi wa mchuano wa kubeba mke
Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.
Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.
Waandaaji wa michuano hiyo wanasema zoezi hilo lilianza mwezi June mwaka 793 AD.
Haki miliki ya pichaPAImage captionMichuano inahusisha umbali wa mita 380 zenye vikwazo kukiwa na miinuko na miteremko
Washindani walikimbia umbali wa mita 15 kupandisha kwenye mwinuko na kushuka ambapo wameeleza kuwa ni kazi ngumu.
Washindani si lazima wawe na ndoa lakini angalau wawe marafiki.
Haki miliki ya pichaPAImage captionChris Hepworth, alimbeba Tanisha Prince, aliibuka mshindi
Sheria inasema wenza wawe na zaidi ya miaka 18 na uzito wa kilo 50 na kuna adhabu ikiwa utamuangusha mwenza wako, ikiwa uzito ni chini ya kilo 50 aliyembeba analazimika kubeba furushi lenye vikopo ili kuongezea uzito.
Mshindi anasema kupanda mlima ilikuwa rahisi kuliko kuteremka.
Washindi wataenda kwenye michuano ya dunia mwezi Julai nchini Finland
Bwana Hepworth ana matumaini ya kushinda.
Haki miliki ya pichaPAImage captionWatu takriban 50 walishiriki
Waandaaji walitoa tahadhari wakisema kuwa ''kumbeba mke kunaweza kuwa jambo la hatari, kunakoweza kusababisha majeraha kama ya uti wa mgongo, kuvunjika miguu na mikono, majeraha usoni, kwenye fuvu la kichwa na hata kifo."
Haki miliki ya pichaPAImage captionBen and Hannah Brackenbury waliingia kwenye michuano hiyo wakiadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao
Ben na Hanna Brackenbury waliingia kwenye mashindano hayo kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya ndoa yao
Wenza hao wamesema walikuwa wakifanya mazoezi kwenye bustani na kwenye mvua wakijiandaa na michuano.
Haki miliki ya pichaPAImage captionMitindo mbalimbali ya kubebana ilishuhudiwa
Mshindi alipata pipa lenye bia anayeshika nafasi ya mwisho anapatiwa tambi na chakula cha Mbwa.
Haki miliki ya pichaPAImage captionWashindi watakwenda kushiriki michuano ya dunia nchini Finland
Haki miliki ya pichaPAImage captionAina hii ya ubebaji imeelezwa iliwafanya wakimbie kwa kasiHaki miliki ya pichaPAImage captionMichuano ya dunia itafanyika mwezi Julai