Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.
Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.
Waandaaji wa michuano hiyo wanasema zoezi hilo lilianza mwezi June mwaka 793 AD.
Washindani walikimbia umbali wa mita 15 kupandisha kwenye mwinuko na kushuka ambapo wameeleza kuwa ni kazi ngumu.
Washindani si lazima wawe na ndoa lakini angalau wawe marafiki.
Sheria inasema wenza wawe na zaidi ya miaka 18 na uzito wa kilo 50 na kuna adhabu ikiwa utamuangusha mwenza wako, ikiwa uzito ni chini ya kilo 50 aliyembeba analazimika kubeba furushi lenye vikopo ili kuongezea uzito.
Mshindi anasema kupanda mlima ilikuwa rahisi kuliko kuteremka.
Washindi wataenda kwenye michuano ya dunia mwezi Julai nchini Finland
Bwana Hepworth ana matumaini ya kushinda.
Waandaaji walitoa tahadhari wakisema kuwa ''kumbeba mke kunaweza kuwa jambo la hatari, kunakoweza kusababisha majeraha kama ya uti wa mgongo, kuvunjika miguu na mikono, majeraha usoni, kwenye fuvu la kichwa na hata kifo."
Ben na Hanna Brackenbury waliingia kwenye mashindano hayo kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya ndoa yao
Wenza hao wamesema walikuwa wakifanya mazoezi kwenye bustani na kwenye mvua wakijiandaa na michuano.
Mshindi alipata pipa lenye bia anayeshika nafasi ya mwisho anapatiwa tambi na chakula cha Mbwa.
No comments:
Post a Comment