Monday, November 6

Kimbunga Damrey chasababisha vifo vya watu 27 Vietnam

Barabara nyingi hazipitiki au ni hatari kupitia Damrey hits Vietnam (04 November 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarabara nyingi hazipitiki au ni hatari kupitia
Kimbunga kwa jina Damrey ambacho kimekuwa kikipiga maeneo ya kusini na kati ya Vietnam kimesababisha vifo vya watu 27, na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko.
Kimbunga hicho kilifika maeneo ya bara Jumamosi kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa.
Nyumba zaidi ya 40,000 zimeharibiwa vibaya na maelfu ya watu wamehamishwa makwao.
Maeneo mengi pia hayana umeme.
Eneo lililoathiriwa zaidi ni jiji la Nha Trang - umbali wa 500km hivi kusini mwa jiji la Da Nang katika pwani ya nchi hiyo ambapo viongozi wa mataifa wanachama wa Apec (Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasific) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu baadaye wiki hii.
People on scooters ride through flood water in Hue city, Vietnam (05 November 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu wakitumia baiskeli kusafiri kupitia barabara za mji wa Hue, Vietnam
Local residents stand inside their flooded home in the tourist town of Hoi An, Vietnam (05 November 2017)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMji wa kitalii wa Hoi An pia umeathiriwa sana
Typhoon Damrey batters a street in Nha Trang, Vietnam (04 November 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMji wa Nha Trang hali imekuwa hivi
Men remove fallen trees on a street in Nha Trang (04 November 2017)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMji ulioanguka na kufunga barabara Nha Trang
Damrey, in Nha Trang (04 November 2017)Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWataalamu wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho ni miongoni mwa vimbunga vyenye uharibifu mkubwa kuwahi kukumba eneo hilo katika miongo kadha
Storm-damaged roof n Ho Chi Minh City (04 November 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPaa la nyumba ambalo limeharibiwa Ho Chi Minh
Map

Trump: Japan itayatungua makombora ya Korea Kaskazini

Bwa. Trump na mwenyeji wake Shinzo Abe, katika ziara yake ya kwanza nchini Japan na Bara Asia kama Rais wa MarekaniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionBwa. Trump na mwenyeji wake Shinzo Abe, katika ziara yake ya kwanza nchini Japan na Bara Asia kama Rais wa Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungusha makombora ya Korea Kaskazini "kuziondoa angani" kwa kutumia mitambo ya kijeshi yaliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litadungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.
Trump aapa kukabiliana na Korea Kaskazini kwenye ziara yake ya Bara Asia.
Alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari leo Jumatatu, Bw Trump alisema kwamba, Bwana Abe atanunua "kiasi kikubwa cha zana za kivita" kutoka Marekani.
Akigusia zana hatari za kinuklea za Korea Kaskazini, Trump alisema kuwa Bw Abe "atazishambulia zikiwa bado angani" mara tu atakapokuwa amemaliza kununua silaha hizo za kijeshi, anazosema kuwa itatoa ajira ya kazi kwa Wamarekani na pia "kutoa usalama kwa Japan".

Mshirika wa Trump Wilbur Ross ahusishwa na kampuni za Urusi zilizowekewa vikwazo

Wilbur Ross has played a key part in Donald Trump's business and political careersHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWilbur Ross amekuwa mtu muhimu katika biashara za Donald Trump na katika siasa zake
Mwanachama wa ngazi ya juu katika uongozi wa Donald Trump anafanya biashara na warusi walio na uhusiano na rais Vladimir Putin, ambao wamewekewa vikwazo na Marekani, kwa mujibu wa ufichuzi wa nyaraka unaojulikana kama Paradise Papers.
Waziri wa biashara Wilbur Ross ana hisa katika kampuni ya Navigator Holdings ambayo hupata mamilioni ya dola kila mwaka kwa kusafirisha mafuta na gesi kutoka kwa kampuni ya mafuta ya Urusi, Sibur.
Wenye hisa wakuu wa kampuni ya Sibur wamewekewa vikwazo na Marekani.
Mtu mwingine mwenye hisa ni mkwe wa rais Putin, Kirill Shamalov.
Graphic showing Wilbur Ross: The Russian connection?
Image captionUhusinao wa Wilbur Ross na Urusi
Ana asilimia 3.2 katika kampuni hiyo. Gennady Timcheno ambaye binafsi amewekewa vikwazo na Marekani ana takriban kampuni 12 zenye uhusiano naye, na Leonid Mokhelson ambaye kampuni yake kuu, Novatek pia imewekewa vikwazo, ni washika dau wakuu.
Msemaji wa wizara ya biasshara alisema kuwa Bw. Ross aliwahi kukutana na washika hau hao watatu wa Urusi.
Marekani ilitangaza vikwazo kadhaa baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea mwaka 2014. Vingine vilitangazwa mwaka uliopita kwa madai ya kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
Ufichuzi huo tena utaibua maswali kuhusu uhusiano wa Urusi na timu ya Trump.
Uongozi wake umekumbwa na madai kuwa Urusi ilihusika katika kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Marekani.
Donald Trump at the Taj Mahal casino in 1990Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump akiwa katika casino ya Taj Mahal casino mwaka 1990
Wilbur Ross na Donald Trump wamejuana kwa zaidi ya robo karne. Bw Ross alishiriki pakubwa katika makubaliano kati ya kampuni ya kamari cha Trump ya Taj Mahal na wakopeshaji wake miaka ya tisini.
Kampuni ya WL Ross & Co ambayo ilianzishwa na Wilbur Ros, mara ya kwanza iliwekeza katika kampuni ya Navigator Holdings mwaka 2011.
Uchunguzi umefichua taarifa kuhusu vile Bw. Ross ni mshika dau katika kampuni ya Navigator Holdings kupitia kampuni kadhaa na visiwa vya Cayman.
Baadhi ya kampuni hizo za Cayman zilifichuliwa na Bw. Ross wakati aliteuliwa waziri wa biashara.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia afariki katika ajali ya ndege

Mei 2015Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege ya vikosi maalum vya Saudia ikipaa Riyadh, 2015
Mwanamfalme mmoja nchini Saudi Arabia amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri pamoja na maafisa kadha wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, runinga ya Al-Ikhbariya imesema.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Saudi Arabia ilisema ilitungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.
Pia, wikendi, watu wengi wakiwemo wana wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.
Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi Mohammed bin Salman.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.
Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadha baada yake kurithi ufalme mwaka 2015.
Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.

Nyaraka za Paradiso: Waziri wa uchumi Marekani ashutumiwa

Wilbur Ross ametekeleza mchango muhimu katika maisha ya Trump ya kibiashara na kisiasaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWilbur Ross ametekeleza mchango muhimu katika maisha ya Trump ya kibiashara na kisiasa
Waziri wa uchumi nchini Marekani Wilbur Ross ameshutumiwa kwa kuwapotosha maseneta nchini humo baada ya nyaraka kuonesha ana uhusiano na Urusi.
Nyaraka hizo ambazo zimefichuliwa, ambazo zinafahamika kama Nyaraka za Paradiso, zimeonesha kwamba amekuwa wakijihusisha na kampuni ambayo ina uhusiano wa kifedha na serikali ya Urusi.
Seneta wa chama cha Democratic Richard Blumenthal ameambia NBC kwamba uhusiano huo ni wa kushangaza.
Nyaraka hizo ambazo zimekabidhiwa kundi la mashirika ya habari, ikiwemo BBC, zinaonesha Bw Ross aliendelea kuwa na maslahi katika kampuni ya usafirishaji wa mafuta na gesi iliyokuwa ikihudumia kampuni ya kawi ya Urusi, Sibur.
Wawili kati ya wamiliki wa kampuni hiyo wamewekewa vikwazo na Marekani na mwingine ana uhusiano wa karibu sana na Rais Vladimir Putin.
Seneta Blumenthal amesema Bw Ross aliambia Bunge la Congress kwamba hakuwa tena na hisa katika kampuni hiyo kwa jina Navigator.
Wizara ya uchumi Marekani imesema Ross hakufanya jambo lolote ambalo ni kinyume cha sheria na kwamba hajawahi kukutana na Warusi hao ambao wamewekewa vikwazo na Marekani.
Graphic - Wilbur Ross; The Russian Connection

Mkutano wa kimataifa wa mazingira waanza Bonn

Mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaanza rasmi leo mjini Bonn, Ujerumani kujadili jinsi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa Paris yanayolenga kuzileta nchi pamoja kupunguza viwango vya joto duniani.

COP23 UN Klimakonferenz in Bonn Eröffnung Salaheddine Mezouar (Reuters/W. Rattay)
Waziri mkuu wa Fiji Voreqe Bainimarama ameufungua rasmi mkutano huo wa Cop23 leo kwa kusema anataka hatua za dharura kuchukuliwa kupunguza gesi chafu inayotoka viwandani kama sehemu ya yaliyofikiwa katika makubaliano ya Paris na hilo linahitaji kila mmoja kuwa na nia njema kulifikia.
Bainimarama ameonya kuwa nchi yake na nchi nyingine za visiwa vya Pacifik ziko katika hatari kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji baharibi na mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa. Na licha ya kuwa Fiji bado haijakumbwa na vitisho vikubwa kama nchi jirani, tayari inakabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
COP23 UN Klimakonferenz in Bonn Eröffnung (Reuters/W. Rattay)
Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, waziri wa mazingira wa Ujerumani Barbara Hendricks amezungumzia umuhimu wa kuyalinda mazingira na kuahidi nchi yake itatoa msaada wa kifedha kuyalinda mazingira.
Takriban watu 25,000 kutoka nchi 195 wanahudhuria mkutano huo wa mazingira unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Ujerumani ndiyo mwenyeji wa mkutano huo wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi ujulikanao Cop23, licha ya kuwa Fiji ndiyo inashikilia urais.
Wanadiplomasia, wanamazingira, wanaharakati, na wanasiasa wanakutana hapa mjini Bonn kwa kipindi cha wiki mbili zijazo kujadiliana ni namna gani watayaokoa mazingira kwa kupunguza viwango vya joto duniani hadi chini ya nyuzi mbili. Kadhalika, makubaliano hayo yanalenga kushajaisha uwezo wa nchi mbali mbali kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Ili kuweza kufikia malengo hayo, kunahitajika fedha za kutosha, matumizi ya teknolokjia mpya, na nchi zinazoendelea kusaidiwa pia kuyafikia malengo yake. Mkutano huo wa mazingira unatarajia kuwa nchi zote husika zitachukua hatua za ziada kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa kikamilifu. Mwaka ujao, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilizotia saini makubaliano ya Paris yatafanya tathmini ya hatua za pamoja zilizofikiwa.
Mkutano huu unaokuja miaka miwili tangu kufikiwa makubaliano ya Paris, unafanyika wakati kuna mashaka baada ya Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Juni mwaka huu kutangaza nchi yake itajiondoa kutoka makubaliano hayo licha ya ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa serikali ya Marekani kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zinashuhudiwa.
COP23 UN Klimakonferenz in Bonn Eröffnung (Reuters/W. Rattay)
Watoto waungana kutaka hatua kuchukuliwa kulinda mazingira
Kimsingi masuala matatu makuu yanayoshughulikiwa ni kuwianisha vipengele vya makubaliano ya Paris, utekelezaji wake na kile kinachojulikana mfumo wa kiutendaji. Ifikapo mwaka 2020 nchi ziwe zimeweza kuimarisha ahadi zake za kupunguza viwango vya joto duniani kwa kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Takriban viongozi 20 wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ni miongoni mwa viongozi mashuhuri watakaohutubia mkutano wa Cop23.
Nchi 49 tayari zimeongeza mikakati yao ya kupunguza gesi chafu inayotoka viwandani na inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, idadi ya nchi ambazo zitakuwa zimepiga hatua inatarajiwa kufika 57, zikiwemo China, Brazil, Marekani na Mexico.
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO litawasilisha ripoti leo katika mkutano wa mazingira wa Bonn inayoonesha kuwa mwaka huu wa 2017 ndiyo unaotajwa kushuhudia viwango vya juu zaidi vya joto duniani kwa zaidi ya nyuzi 1.1 hiyo ikiwa hali mbaya ya hewa ambayo haikutarajiwa.

WAZIRI AAGIZA UCHUNGUZI VYOO GEREZA LA ISANGA

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni, amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira kuunda tume  kuchunguza Sh milioni 70 zilizotolewa na Serikali kujenga vyoo katika Gereza la Isanga mkoani hapa.
Pia amepiga marufuku ujenzi wa nyumba katika eneo la gereza hilo.
Akizungumza jana akiwa   gerezani hapo, Masauni alisema kuna taarifa ya kuwapo ubadhirifu wa Sh milioni 70 zilizotolewa na Serikali kwa ujenzi wa vyoo vya 32 katika gereza hilo.
“Kwamba inasemekana kuna ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya Magereza ya Isanga.
“Namwagiza Katibu Mkuu kuunda tume  ifanye uchunguzi  tuweze kupata majibu na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaobainika kuhusika,” alisema.
Masauni alishangaa mradi huo kuchukua zaidi ya miaka mitatu na kuhoji ni kwa nini umechukua muda mrefu kukamilika.
Naibu Waziri pia amepiga marufuku ujenzi wa nyumba katika eneo la gereza hilo hadi  uchunguzi utakapokamilika ni nani mmiliki halali wa eneo hilo.
Inadaiwa  baadhi ya watu wakiwamo watendaji wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) walijigaia viwanja na kujenga katika eneo hilo la gereza.
“Kipindi hiki wakati haya maelekezo yanafanyika ni marufuku kwa mtu yeyote kuendeleza ujenzi katika eneo hili awe na kibali, awe hana, kiwe cha kweli au cha uongo, hili ni jeshi.
“Nimeishaagiza askari magereza wamshughulikie yeyote ambaye atakuja kufanya shughuli za ujenzi katika eneo hili kabla jambo hili halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu,” alisema.

SIRI BOMBERDIER NJE

SERIKALI imesema ifikapo Julai  mwakani, ndege zote zilizoagizwa zitakua zimeingia nchini tayari kuanza kazi.
Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dk. Hassan Abbasi, amesema kwa sasa Serikali imejipanga   kuleta   ndege hizo na zitawasili Juni 2018.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana kuhusu mafanikio ya miaka miwili ya Rais Dk. John Magufuli madarakani tangu alipoapishwa Novemba 5, mwaka 2015.
Dk. Abbasi ametoa kauli hiyo huku hadi sasa ikiwa haijaelezwa  hatima ya kesi  ya ndege   ya Bombardier Q400 Dash 8, ambayo inadaiwa kuzuiwa  Canada kutokana na serikali kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kimataifa ya kulipa fidia.
Hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICSD) iliyotolewa mwaka 2010 iliitaka Serikali kuilipa kampuni ya ujenzi ya Stirling Civil Engineering Ltd dola  za Marekani milioni 25   na riba ya asilimia nane (Sh bilioni 87).
Kuhusu kesi zinazoikabili  Serikali, Dk. Abbasi, alisema kuna kesi mbili bila kutaja za aina gani;   moja ambayo Serikali imeshtakiwa na nyingine imeshtaki na   ipo katika hatua nzuri.
“Ndege kubwa kuliko zote itaingia Julai 2018 ambayo ndiyo ndoto ya serikali na kuhusu kesi siwezi kufahamu zote kwa sababu  kuna nyingine ni za  binafsi ingawa Tanzania imeshitaki na wao wameshitaki na na ipo katika hatua nzuri,” alisema.
Dk. Abbasi alisisitiza kuwa  ndege zote zilizoagizwa zikiwamo  Boeing 787, Bombardier CS300, Boeing 787 – 1 abiria 262 Bombardier 400 – 3 abiria 76, Bombardier CS300 – 2 abiria 132, zote zitaingia mwezi Juni.
Alisema dhamira ya serikali ni kulifufua Shirika la Ndege  na imefanya hivyo.
“Tunafufua Shirika la Ndege, tumeanza na juhudi hizo …  hadi kufikia mwakani ndege zote tulizoagiza zitakuja na hiyo uliyoitaja ipo kwenye  majaribio kwa maana ya vipimo na kufanyiwa ukaguzi, itakapokamilika itakuja nchini,’’ alisema.
WAFANYAKAZI HEWA
Msemaji huyo wa serikali pia alielezea mafaniko mengine kuwa ni pamoja na kudhibiti ufujaji wa fedha za umma hasa kwenye suala la wafanyakazi hewa ambako iliwaondoa  katika mfumo wa malipo wafanyakazi hewa takriban 20,000 na kuokoa  Sh bilioni 238.
Alisema wafanyakazi wenye vyeti feki takribani 12,000 wameondolewa katika mfumo wa serikali na kuokoa    Sh bilioni 142.9.
Hata hivyo akijibu swali la kuhusu uamuzi wa kusimamisha  ajira za watumishi wa kada ya afya waliopangiwa vituo vya kazi hivi karibuni katika halmashauri mbalimbali, alisema hatua hiyo inatokana na kufanya uhakiki na marekebisho na baada ya kukamilika zitatangazwa tena hivi karibuni.
Alisema marekebisho hayo ni pamoja na ukaguzi wa taaluma ili yasiweze kurudiwa makosa ya kuwa na wafanyakazi hewa na vyeti feki na baada ya hapo yatatangazwa tena.
VITA YA UFISADI
Alizungumzia mafanikio ya vita ya ufisaidi akisema ni pamoja na kuanzishwa kwa mahakama ya ufisadi na  kufanya usimamizi wa fedha za umma kuhakikisha zinazopatikana kutokana na jasho la walipakodi zinatumiwa ipasavyo ili kuleta faida kwa wananchi.
Alisema mahakama ya ufisadi imeanza kazi  kwa kasi kwa kuanzia mahakama za chini  zikiwamo kesi za  uhujumu uchumi katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mikoa mengine mbalimbali na hadi sasa kuna kesi 104.
Dk. Abbasi alisema kesi zenye maombi ya dhamana yaliyokamilishwa na kupelekwa mahakama ya uhujumu uchumi kwa uamuzi ni 77 na   tatu zimeanza kusikilizwa katika mahakama hizo.
MAZUNGUMZO MAKINIKIA
Mafanikio mengine  ni   mazungumzo ya historia na kampuni ya  Barrick    kwa kuwa katika mabadiliko yaliyofanyika, taifa  kwa sasa litapata hisa asilimia 16 na mgawanyo wa asilimia 50/50 wa faida katika migodi ya madini.
“Mazungumzo katika maeneo mengine kama Tanzanite na almasi yanakuja lakini tayari uzalishaji umeongezeka kutoka karati kati ya 15,000-18,000 hadi karati kati ya 28,000 na 32,000,’’ alisema Dk. Abbas.
SAFARI ZA NJE 
Msemaji huyo wa serikali, alisema serikali imefanikiwa kufuta safari za nje ya nchi sisizo za msingi    na matumizi yasiyokuwa ya msingi kwa viongozi na maofisa  wa umma yameshuka.
Alisema kwa mwaka 2014 -2015 takribani Sh bilioni 216 zilitumika  kwa mambo kama hayo   lakini kwa mwaka 2015 -2017 Sh bilioni 25 tu   zimetumika hadi sasa.
Aliyataja mafanikio mengine   aliyoita ya uamuzi mgumu  ambayo ni pamoja na kitendo cha serikali kuhamia Dodoma, ndoto aliyoiita ni ya miaka 44 iliyopita ambayo utekelezaji umefanyika sasa.
Mafanikio mengine  ni katika makusanyo ya kodi ambayo kwa mwaka  yameongezeka mwezi.
Alisema  hadi kufikia Juni mwaka huu zilikuwa zimekusanywa  Sh trilioni 15 zilikusanywa wakati mwaka 2015 zilikusanywa Sh trilioni 9.9.
Dk. Abbasi alisema kutokana na makusanyo hayo,   bajeti imeongezeka katika sekta zote hasa miradi ya maendeleo na  katika miaka miwili limekuwapo ongezeko la asilimia 40.
Alisema ongezeko hilo  ni kwenye sekta ya afya kwenye dawa na vifaa tiba ambako mwaka huu bajeti imekuwa Sh bilioni 261 wakati mwaka 2015 ilikuwa Sh bilioni 30.
“Mwaka 2016 serikali ilitenga  Sh bilioni 251 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba na yote ilitolewa katika vituo 268 vya afya wakati Hospitali ya Taifa Muhimbili imepata  CT-Scan mpya na hivi sasa inasaidia wagonjwa 50 kutoka 20 kwa siku.
“Bila kusahau elimu bure   serikali ikiwa inatoa Sh bilioni 20 kwa mwezi kugharamia ada, posho za wakuu wa shule, uendeshaji wa shule na chakula   na  Sh  bilioni 3 kwa ajili ya kugharamia mitihani ya  darasa la nne, saba, Form II na Form IV,   jumla zikiwa Sh bilioni 23,’’ alisema Dk. Abbasi.
Akizungumzia mafanikio katika elimu ya juu, alisema Serikali  inagharamia wanafunzi wenye uhitaji wa elimu ya juu kwa ada, matumizi na vifaa kwa   Sh bilioni 427 kutoka Sh bilioni 48.6 za mwaka 2015/16.
Alisema  kwa mwaka huu pekee wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa wameongezeka kutoka 28,785 hadi 30,000.
MIRADI YA MAJI
Kuhusu  miradi ya maji, alisema zimekwisha kutumika Sh bilioni 550   kwa ajili ya kutoa maji Ziwa Victoria kwenda mikoa ya Tabora na jirani.
“Na pia   mradi wa maji Arusha umetumia Sh  bilioni 476  na katika miji 17 na Zanzibar miradi ya maji imegharimu Sh trilioni 1.2,” alisema.
BARABARA
Alisema Serikali imejenga takribani kilometa 1,500 za barabara na kutumia Sh trilioni 1.2 ambazo zote ni fedha za ndani, sambamba na ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia trilioni 1.9.
UMEME
Dk. Abbasi alisema kuwa pia Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi ya historia ya umeme ambayo ni Kinyerezi I Extension ambayo mtambo wake unazalisha Megawati 185 za umeme ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa  ifikapo Novemba 2018.
UWEKEZAJI
Msemaji huyo wa serikali  alisifu maendeleo ya uwekezaji  nchini hasa katika kutekeleza sera ya ‘Tanzania ya Viwanda’ kama vile  kuanzishwa Kiwanda cha Chaki Maswa, Kiwanda cha Sayona Mwanza na vingine vingi.

Watu 26 wauawa kanisani Texas Marekani

Askari na wafanyakazi wa dharura wakiwa katika eneo la mauaji katika kanisa la First Baptist huko Sutherland Springs, Texas, Nov. 5, 2017.
Mtu mmoja anayeaminika kuwa mwanajeshi wa zamani wa jeshi la anga la Marekani aitwaye Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26 ameshambulia watu kwenye kanisa moja karibu na San Anrtonio jumapili asubuhi na kuuwa watu 26 na kujeruhi wengine wasiopungua 20.
Walioathirika katika shambulio hilo la kanisani kwa silaha nzito za risasi za mauaji ya halaiki ni kati ya umri wa miaka 5 hadi 72.
Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na bado haijulikani sababu ya kuchukua hatua hiyo.
Wachunguzi kutoka idara ya makosa ya jinai FBI na idara ya usimamizi wa vilevi, tumbaku na silaha wako Sutherland Springs Texas kiasi cha kilometa 50 kutoka San Antonio.
Rais Donald Trump ameita mauaji hayo kitendo cha kikatili na kutoa wito wa maombi. Rais anafuatilia hali ilivyo akiwa Japan kituo chake cha kwanza katika ziara ya nchi 5 za Asia .

Mmarekani ashinda marathon za New York kwa mara ya kwanza katika miaka 40

Geoffrey Kamworor wa kenya akimaliza mbio za Marathon za New York, Nov. 5, 2017.
Shalane Flanagan kwa mshangao amemshinda bingwa wa mara tatu wa mbio za marathon za New York, Mary Keitany kutoka Kenya siku ya Jumapili na kuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani kushinda mbio hizo.
Kwa upande wa wanaume wakenya waliwika pale Geoffrey Kamworor aliponyakua ushindi wake wa kwanza na kumshinda mwenzake Wilson Kipsang bingwa wa dunia wa mbio hizo kwa sekunde tatu.
Keitany alishashinda mara tatu mfululizo mbio hizo maarufu, lakini Flanangan mwenye umri wa miaka 36 alimpita Mkenya huyo kiasi cha maili tatu kabla ya kumalizika mbio na hakumona tena hadi mwisho akitumia saa 2 dakika 26 sekunde 53.
Mara ya mwisho kwa mwanamke Mmarekani kushinda mbio hizo za New York alikua Miki Gorman aliyenyakua taji mara mbili mfululizo 1976 - 1977.

Sunday, November 5

Vigogo 11 wakamatwa Saudi Arabia

Serikali ya Saudi Arabia imewakamata vigogo kadhaa wakiwemo wana wa kifalme, mawaziri na wafanyabiashara wakubwa katika kile inachosema ni vita dhidi ya ufisadi vinavyoongozwa na mrithi wa kiti cha ufalme.

König Salman Bin Abdul Aziz Al Saud und Kronprinz Mohammed Bin Salman Al Saud (picture-alliance/abaca/B. Press)
Bilionea mkubwa, Al-Waleed bin Talal, ni miongoni mwa wana wa kifalme 11 waliokamatwa usiku wa jana (Jumamosi, 4 Novemba 2017), mara tu baada ya kamisheni mpya ya kupambana na ufisadi inayoongozwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman kutangazwa kwa amri ya kifalme.
Katika tukio jengine, mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Taifa, ambaye aliwahi kuwa mmoja wa waliotazamiwa kurithi kiti cha ufalme, na pia mkuu wa jeshi la pwani na waziri wa uchumi waliondolewa kwenye nafasi zao, ikiwa sehemu ya wimbi la ufutwaji kazi katika Ufalme wa Saudia.
Kituo cha televisheni cha Al Arabiya kinachomilikiwa na Saudi Arabia kiliripoti kwamba wana wa kifalme hao, mawaziri wanne wa sasa serikalini na mawaziri wengine kadhaa wa zamani walikamatwa, huku kamisheni hiyo ikianza uchunguzi juu ya visa vya zamani kama vile mafuriko yaliyoukumba mji wa Jeddah mwaka 2009.
Shirika la habari linalomilikiwa pia na serikali ya Saudia, SPA, lilisema lengo la kamisheni hiyo ni "kulinda fedha za umma, kuwaadhibu mafisadi na wale wanaoutumia vibaya nafasi zao."
Hisa zaporomoka
Billionär Al-Waleed Bin Talal bin Abdulaziz al Saud (Getty Images/AFP/I. S. Kodikara)
Bilionea Al-Waleed Bin Talal bin Abdulaziz al Saud
Hisa kwenye kampuni ya Kingdom Holding, ambazo zinamilikiwa kwa asilimia 95 na Mwanamfalme Al-Waleed, zilishuka kwa asilimia 9.9 wakati maduka ya hisa yalipofunguliwa asubuhi ya Jumapili, kukiwa tayari na taarifa za kukamatwa kwake.
Ofisi yake haikupatikana mara moja kuzungumzia suala hili.
"Kwa msako huu, ufalme unaanza enzi mpya na sera ya uwazi, usafi na uwajibikaji," alisema Waziri wa Fedha wa Saudi Arabia, Mohammed al-Jadaan, kwa mujibu wa shirika la habari la SPA.
"Maamuzi haya magumu yatalinda mazingira ya uwekezaji na kuinua imani kwenye utawala wa sheria."
Baraza kuu la maulamaa la nchi hiyo liliisifia pia hatua hiyo kuwa ni "muhimu", kauli ambayo inachukuliwa kama baraka za kidini kwa msako huo. 
Chanzo kimoja kutoka usafiri wa anga kililiambia shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya usalama vimezizuwia ndege binafsi kuruka kutoka viwanja vyote vya ndege vya nchi hiyo, yumkini ikikusudiwa kuwazuwia vigogo kukimbia nchi.
Hatua hizi za kushitukiza zinakuja katika wakati ambapo taifa hilo lenye uhafidhina wa kiwango cha juu likianzisha mageuzi makubwa kwenye masuala ya kijamii na kiuchumi, kufuatia kutangazwa kwa Mwanamfalme Mohammed kuwa mrithi rasmi wa nafasi ya baba yake, Mfalme Salman, ambaye alimuondoa kwenye mstari wa urithi binami yake, Mwanamfalme Mohammed bin Nayyaf, aliyemuweka kwenye kizuizi cha ndani tangu mwezi Juni.