Tuesday, August 1

WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAENDELEA NA MAFUNZO KUHUSU UDHIBITI WA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA UTENDAJI WA VYUO MKOANI MOROGORO


Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Mwenyekiti wa Mafunzo Bw. Paschal Mahinyila akiwakaribisha washiriki katika mafunzo Wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti mkoani Morogoro leo tarehe 01.08.2017. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike (kushoto) akifafanua umuhimu wa uadilifu kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii(hawapo pichani) katika utendaji kazi wa vyuo wakati wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Uendeshaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani(kulia) akifafanua mambo mbalimbali ya kiutawala kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo.
Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Fatuma Oloo(kulia) akisisitiza jambo kuhusu udhibiti wa fedha kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Martha Chuma (katikati) akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo ugavi na manunuzi kwa wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao(kulia) akitoa maelekezo kuhusu mikataba na masuala mbalimbali ya kisheria kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkaguzi wa ndani kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Elightness Mchome(katikati) akifafanua umuhimu wa kuepuka hoja za ukaguzi kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayoendelea katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Salim Mgalla(kulia) akiuliza swali kwa wawezeshaji katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro
Baadhi ya wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii Nchini wakifuatilia wawasilishaji mada(hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mratibu wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi Bw. Moris Jackson akifafanua masuala mbalimbali yahusuyo Viashiria Hatarishi kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya Jamii Nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Kaimu Mkuu wa Chuo (Utawala, Mipango na Fedha) Kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha Bi.Nadhaherieth Mshighath akiuliza swali kwa wawasilishaji mada (hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Watendaji kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na washiriki kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 01.08.2017. 

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI PIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATANO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn mara baada  ya kumaliza mazungumzo pamoja na kupokea Hati za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn katikati akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimshukuru Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati zake Utambulisho.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kupokea hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Tumisiime Kabonero Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipiga ngoma ya Brass Bendi ya Jeshi la Polisi ambayo ilifika Ikulu kwa ajili ya mapokezi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Brass Bendi ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Marekani yazuia mali za Maduro


 Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi uliokumbwa na mgogoro Venezuela, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa taarifa kutishia kumchukulia kiongozi wa taifa hilo hatua nzito na za haraka.
Kwa kuanzia imezuia mali zote anazomiliki Maduro nchini Marekani na Waziri wa Fedha Marekani, Steven Mnuchin, amemtaja Maduro kuwa dikteta.
"Uchaguzi unathibitisha Maduro ni dikteta asiyezingatia matakwa ya raia wa Venezuela," amesema katika taarifa yake.
Hii si mara ya kwanza kwa marekani kuchukuwa hatua dhidi ya viongozi wa serikali hiyo , huku viongozi wakuu 13 wa utawala wa Maduro wakilengwa kwa vikwazo kama hivyo vilivyotangazwa wiki iliopita.

Dar yaongoza mauaji ya kujichukulia sheria mkononi

Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fundikila Wazambi (kushoto) akifafanua kuhusu ripoti ya nusu mwaka ya haki za binadamu iliyozinduliwa na kituo hicho jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dkt Hellen Kijo Bi-Simba na Mkurugenzi wa Ufatiliaji Ukiukwaji Haki za Binadamu na Uwajibikaji, Felista Mauya. Picha na Ericky Boniphace 
 Kwa kawaida vyombo vya habari vimezoea kuwaita wanaofanya mauaji kwa kujichukulia sheria mkononi kuwa ‘watu wenye hasira kali’.
‘Wenye hasira kali’ hao wamekatisha uhai wa watu 479 kuanzia Januari mpaka Juni mwaka huu.
Mkoa wa Dar es Salaam unatajwa kuwa kinara kwa matukio ya mauaji yanayotokana na wakazi wake kujichukulia sheria mkononi.
Hali hiyo ilibainishwa jana jijini hapa na Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fundikira Wazambi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi Juni, 2017.
“Katika ripoti yetu tumebaini ndani ya kipindi hicho watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi.
Alinukuu ripoti ya polisi kuwa jumla ya watu 479 wameuawa nchini kutokana na watu kujichukulia sheria mkononi.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa matukio hayo kwa kuwa na vifo 117, ukifuatiwa na Mbeya (33), Mara (28) na Geita (26).
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Helen Kijo Bisimba alisema kituo hicho pia kimepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kuteswa na wengine wameuawa kwa tuhuma za mauaji yanayofanyika Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani.
“Kuna vifo tisa ambavyo vinahusisha vyombo vya dola, ingawa Jeshi la Polisi katika taarifa yake inaonyesha ni mtu mmoja pekee ndiyo aliuawa akiwa mikononi mwa polisi,” alisema.
Akizungumzia hali ya usalama wa watoto alisema kuna unyanyasaji mkubwa na matukio ya ukatili hasa wa ngono na hadi Juni matukio 121 yameripotiwa.
Kutokana na matukio hayo, LHRC imetoa ushauri kwa Serikali na Bunge kushughulikia kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sheria.
Dk Bisimba alisema kuna mambo kadhaa yanayotendeka nchini kinyume cha haki za binadamu na sheria.
“Ripoti inaonyesha kuwa hali ya haki za binadamu ni mbaya kwa kipindi cha nusu mwaka 2017 ikilinganishwa na miaka iliyopita, hii imesababishwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kiraia na za kisiasa, hususani haki ya kuishi na kuminywa kwa uhuru wa kujieleza,” alisema Dk Bisimba.
“Kutokana na hayo tuliyobaini tuna mapendekezo mengi ikiwamo, Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha sheria zinazobana uhuru wa kujieleza kama huduma ya habari na sheria ya makosa ya mtandaoni zinafanyiwa marekebisho haraka,” alisema.

Mkuu wa wilaya awasamehe waliopopoa mawe msafara wake


 Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, amewasamehe wanakijiji wa Mlongia kata ya Jongolo waliobeba silaha za
kijadi, virungu na mawe wakidaiwa kuupiga mawe msafara wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo ulipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi
katika kijiji hicho.
Akizungumza jana Jumatatu, Odunga amesema ameamua kuwasamehe na kutowafikisha mahakamani wakazi hao wanaodaiwa kuhusika katika vurugu hizo baada ya makubaliano kuwa hawatarudia tena kitendo kama hicho.
“Haina haja ya kuendelea na ugomvi na wananchi ambao unawaongoza.
Niliwasamehe na waliapa kutorudia tena vitendo kama hivyo na sasa hali
imetulia,” amesema Odunga.
Tukio hilo lilitokea Januari mwaka huu wakati Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya hiyo ilipokuwa ikenda katika mkutano huo uliolenga
kujadili mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa kijiji hicho na mwekezaji
aliyetambulika kwa jina la Msukuma, ambaye anadaiwa kupewa ekari 500
kwa ajili ya kuwekeza katika eneo la kijiji hicho.
Kwa mujibu wa Odunga, hakuna haki ambayo imekiukwa na mwekezaji
huyo bali mvutano huo ulitengenezwa na wanasiasa.
“Hakuna haki ya msingi ambayo imekiukwa katika eneo hilo isipokuwa
mgogoro huo umesababishwa na elimu ndogo na wanasiasa  kuwachochea
wananchi,” alisema.
Alisema kimsingi shamba hilo la mwekezaji lenye ukubwa wa ekari 450 liko katika kijiji cha Kwadelo wilaya ya Kondoa na wala si wilaya ya Chemba.
“Na viongozi wa Wilaya ya Kondoa wanamtambua mwekezaji huyo lakini
wanasiasa hawa wamekuwa wakimpiga vita tangu mwaka 2006, sijui ni
kwa sababu gani,” alisema.
Katika tukio hilo, wanakijiji hao wakiwa na silaha za jadi, mapanga,
virungu na mishale walishambulia Kamati ya Ulinzi na Usalama na
kuharibu pia gari ya Mkuu wa Usalama wa Wilaya baada ya kulipiga mawe.
Tukio hilo lilisababisha watu 30 kukamatwa akiwemo mwenyekiti wa
kijiji na kuhojiwa kuhusiana na fujo hizo.a

Kesi ya Malinzi, Aveva zapigwa kalenda


 Kesi inayowakabili viongozi  Shirikisho la Soka nchini, rais wa TFF, Jamal Malinzi, Katibu wake Celestine Mwesigwa na mhazini Nsiende Mwangwa imehairishwa hadi Agosti 11.
Kusogezwa mbele kwa kesi hizo ni baada ya mawakili upande wa Jamhuri kuomba tarehe zingine kwa upelelezi wa mashauri hayo haujakamilika.
Malinzi na wenzake wanashtakiwa kwa makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha.
Wakati kesi ikipangwa kusomwa tena Agosti 11, upandwa wa viongozi wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geoffrey Kaburu zimepigwa kalenda hadi Agosti 7.
Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alisema kesi hiyo Aveva na Nyange inahitaji upelelezi wa muda mrefu kutokana na asili ya mashitaka yake.
"Mahakama haina mamlaka ya kuifuta kwa siku 60, hivyo wanatoa tarehe fupi ili upande wa mashitaka ufanye kazi ya kukamilisha upelelezi."
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili Aveva na Kaburu ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.
Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
Shtaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya  Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha  likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.

Amuua mumewe kisa amewahi kuingia bafuni


Mgini Aron (37), mkazi wa Magunga Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mkewe Jeni Mwenda (25) kwa sababu ya wivu wa mapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Jumatatu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 30 majira ya saa 11:15 jioni katika kitongoji cha Kitaramanka, Kata ya Mirwa.
Alisema baada ya marehemu kutoka matembezini alifika nyumbani moja kwa moja na kuingia bafuni kitendo kilichomkasirisha mkewe akidai kwanini amerudi na kuingia bafuni moja kwa moja.
Kamanda Mohamed alisema kuwa baada ya marehemu kuambiwa hivyo walianza ugomvi na mpenzi wake huyo, katika purukushani za hapa na pale ndipo Jeni alipomchoma na kitu chenye ncha kali upande wa titi la kushoto na kusababisha kifo chake.
Kamanda alisema mtuhumiwa ameshakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa uchunguzi zaidi.

Makani asisitiza utalii wa misitu


Serikali imesema itaimarisha utalii wa misitu ya asili nchini ili iweze kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa tofauti na hali ya hivi sasa ambapo utalii hutegemea zaidi wanyamapori.
Hayo yamesemwa leo Jumanne wilayani Lushoto na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua migogoro mbalimbali katika maeneo ya uhifadhi.
Alisema sekta ya utalii nchini imekuwa ikitegemea sana wanyamapori na kusahau vivutio vingine kama vile misitu ya asili ambayo ndani yake kuna mimea na viumbe hai mbalimbali adimu duniani na ambavyo hupatikana Tanzania pekee.
“Tumezoea zaidi utalii wa wanyamapori… lakini utalii wa misitu unaweza kuzidi hata wa wanyamapori. Kwenye misitu yetu ya asili tunajivunia mimea adimu ya asili na viumbe hai mbali mbali kama vile ndege, vyura, vipepeo, mijusi na kadhalika. Tunachotakiwa kufanya ni kutunza misitu yote ya asili, tuiboreshe na kuitangaza ili kupata watalii wengi zaidi na pato la Taifa liendelee kukua,” alisema Makani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Tanzania ina jumla ya Hifadhi za Misitu ya Asili 100, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na hifadhi za taifa ambazo zipo 16 pekee. Pamoja na upekee wake, idadi hiyo kubwa inatoa fursa pana ya kuendeleza sekta ya utalii nchini.
Akizungumzia mafanikio, Makani alisema sekta hiyo inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.
Alisema pamoja na faida hizo, sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wa misitu ya asili ambayo ni muhimu kutafutiwa suluhu ya kudumu ili kunusuru misitu hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari Lugangika, alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ya asili, uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya hifadhi, uchomaji moto misitu na uhaba wa watumishi.
Katika ziara yake hiyo wilayani Lushoto, Naibu Waziri Makani alitembelea pia Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba na Shamba la Miti la Shume.

Serikali yawaonya waajiri kuhusu wafanyakazi wanaonyonyesha


Serikali imeonya waajiri wanaoweka vikwazo kwa wafanyakazi wao wanaonyonyesha watoto walio chini ya miezi sita.
Onyo hilo limetolewa leo Jumanne na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati anafungua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.
"Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora, imeweka kanuni inayompa nafasi ya saa mbili mama mwenye mtoto wa chini ya miezi sita kumnyonyesha mwanaye," amesema Waziri Mwalimu. 
Amesema kutokana na kanuni hiyo, waajiri wanapaswa kuwapa ushirikiano mzuri akina mama hao, kwa kuwa maziwa ya mama ndiyo msingi wa afya bora ya mtoto.
Waziri Mwalimu amebainisha kuwa ili mtoto aweze kuwa na afya bora, anapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita mfululizo bila kinywaji au chakula kingine chochote.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Chakula na Lishe, Dk Joycline Kaganda, amesema maadhimisho haya hufanywa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi 7. 
"Maadhimisho haya yanalenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama," amesema
Katika maadhimisho hayo, programu ya huduma ya taarifa za lishe kupitia simu za mkononi (M-Nutrition) imezinduliwa. Progrtamu hiyo inakusudia kuleta mabadiliko ya tabia kuhusu afya na lishe ya watoto, wanawake wajawazito  na wanyonyeshao.

Zimamoto wazindua namba mpya ya dharura



Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, likishiriakiana na asasi ya kiraia iitwayo United Against Crime, wamezindua kampeni ya kuitangaza namba mpya - 114 - ya dharura kwa ajili ya kupiga pindi yanapotokea majanga mbalimbali yakiwamo ya moto.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumanne Agosti Mosi makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam na umekwenda sanjari na kuhamasisha Watanzania kufahamu kwa undani majanga ya moto na namna ya kukabiliana nayo
Kamishana Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye, amewaambia wanahabari kuwa namba hizo zitawasaidia Watanzania kupiga simu na kupatiwa huduma za uokozi haraka.
"Watu wengi wanaifahamu namba 112 ambayo ni polisi lakini 114 hawaifahamu vizuri, hali inayosababisha kutumia muda mwingi kupiga 112 badala  ya 114. Nina imani sasa hivi watakuwa wanaitumia  namba hii," anasema Kamishna Andengenye.
Amesema uzinduzi huo wa kampeni unakwenda sambamba na mchakato wa kuwajengea uewela Watanzania wa namna ya hatua za kuchukua na kukabiliana na majanga ya moto
Katibu Mtendaji wa United Against Crime, Andrew Elliot amesema wameamua kuweka nguvu katika kampeni ili kuokoa Watanzania na majanga ya moto na kwamba kupitia mchakato huo Watanzania watajengewa uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga hayo.
Elliot amesema katika kampeni hiyo wamesharikiana na watu mbalimbali ikiwamo kampuni ya Mabati ya Alfa na Selc

Monday, July 31

WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI


WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.
Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.
Ameyasema hayo Jumapili, Julai 30, 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.
Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.

“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”
Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku.

Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.

Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto.

Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija. 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Mhe. Amos Makalla. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha gesi cha TOL Gases Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Baada ya kuwasili kiwandani hapo Julai 30, 2017 Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai 30, 2017. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Mhe. Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Ramadhani Kampasili. 
Waziri Mkuu  Mhe. Kassim Majaliwa akitazama chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017.  
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe baada ya kutembelea kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri (kulia Kwake) kuhusu mitambo ya kuzalisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa kijiji cha Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya Kimyakyusa iitwayo "Ndigala" baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo mkoani Mbeya kuhutubia mkutano wa hadhara 
Sehemu ya watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozungumza nao leo Julai 30, 2017.