Nyumba 15 zilibomolewa Desemba 3 mwaka jana baada ya kudaiwa kujengwa ndani ya hifadhi ya msitu wa kuni uliopo mpakani mwa Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro. Akizungumza na wakazi wa mtaa huo jana, mbunge huyo alisema baada ya uongozi wa manispaa kuketi na wahusika ambao ni idara ya misitu ilibainika eneo lililobomolewa kwa makosa.
Mmoja wa wakazi hao, Nashir Kamgisha licha ya kumpongeza mbunge huyo kwa juhudi zake, alimuomba kuwasaidia kupimiwa viwanja ili kuondokana na changamoto ya makazi holela.
Hivi karibuni, ofisa mipango miji wa Manispaa ya Morogoro, Steven Balozi alieleza kusitishwa na bomoabomoa na sasa wanapitia upya mipaka ya Mvomero na manispaa.
No comments:
Post a Comment