Sunday, April 1

Mapya yaibuka ujio wa Zari, kuvuna mamilioni


Dar es Salaam.Mrembo Zarinah Hassani ‘Zari’ inaelezwa alikuwepo nchini siku nne zilizopita.
Akizungumza na Mwananchi mmoja wa wenyeji wa Zari ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alisema mrembo huyo alifika nchini siku tatu zilizopita kabla ya kukutana na waandishi wa habari ambapo alitangazwa rasmi kuwa balozi wa nepi za watoto za softcare zinazotengenezwa na kiwanda cha Keds Tanzania.
Chanzo hicho kilieleza kwamba tangu mama huyo wa watoto watano afike nchini alitumia muda mrefu kupiga picha kwa ajili ya tangazo litakaloonekana katika nepi hizo.
Alisema Zari aliyezaa watoto watatu na msanii nyota nchini Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitumia muda mrefu nchini ili kumzoea mtoto ambaye ataonekana naye kwenye tangazo. “ Tangazo hili alitakiwa kufanya na mwanaye Tiffah, lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo imebidi atafutwe mtoto mwingine,” kilisema chanzo hicho.
Zari aliyevunja uhusiano na Diamond, juzi alipata mkataba mnono wa miaka mitatu wa nepi za watoto ambazo zinatoka China.

No comments:

Post a Comment