Katibu tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, ametoa taarifa hiyo leo Machi 15 katika Kikao cha Kamati ya UshauriM(RCC) ya mkoa wa Arusha na kueleza kuwa hadi sasa bado kuna watu wameendelea kuugua ugonjwa huo.
Kwitega amesema ugonjwa wa Kimeta umekuwa ukitokea na kwa kujirudiarudia mkoani Arusha, na kwamba Novemba mwaka juzi ugonjwa huo ulianza kuripotiwa wilayani Monduli .
"Ugonjwa huu ulitokea katika kata ya Selelana kusababisha vifo vya wanyamapori pamoja na mifugo na kuleta madhara kwa baadhi ya watu," amesema
Hata hivyo, amesema kuna jitihada zinaendelea katika kupambana na ugonjwa wa kimeta.
Amesema Mkoa wa Arusha unay timu ya afya moja (one Health Team) ambayo inajumuisha wataalamu wa mifugo na afya kwa kuzishirikisha wilaya katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo.
"Jitihada zimekuwa zikikabiliwa na changamoto za ufinyu wa bajeti kwa ajili ya mafuta, posho na vifaa hivyo kukwamisha utekelezaji kwa maana ya mafunzo, tiba na chanjo na ufatiliaji wa kina katika jamii," amesema.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wakazi wa Arusha, Joram Lazier na Edna Joseph, wameiomba, Serikali kuongeza kutoa elimu juu ya ugonjwa wa kimeta ili kukinga wasiugue.
"Huu ni ugonjwa unatoka kwenye mifugo kwenda kwa binaadamu hivyo, tunaomba tu elimu zaidi,"amesema
Kwa upande wake Joseph amesema bado wananchi wengi hasa wa vijijini hawajuwi dalili za ugonjwa huo na hatua za kuchukuwa mara baada ya kuugua.
No comments:
Post a Comment