Friday, March 16

Utafiti: Vipande vya plastiki vyapatikana katika maji ya chupa

Baadhi ya chupa zilizofanyiwa uchunguzi
Image captionBaadhi ya chupa zilizofanyiwa uchunguzi
Vipimo vya maji yanayouzwa katika chupa za plastiki vimebaini kwamba maji hayo yana vipande vidogo vya plastiki ndani yake.
katika uchunguzi mkubwa kuwahi kufanyika duniani kuhusu maji hayo , chupa 250 zilizonunuliwa kutoka mataifa 250 zilichunguzwa.
Utafiti ulioongozwa na shirika la wahandishi habari Orb Media ulibaini vipande 10 vya plastiki katika lita moja ya maji ,ikiwa ni ukubwa wa upana wa unywele wa binadamu.
Kampuni ambazo maji yao yalichunguzwa ziliambia BBC kwamba chupa zao za maji zilitengezwa kwa ubora wa hali ya juu. Vipimo hivyo vilifanywa katika chuo cha kitaifa cha New York huko Fredonia.
Sherri Mason ambaye ni profesa wa kemia katika chuo kikuu alifanya uchanganuzi huo na kuambia BBC ''tulipata plastiki katika chupa baada ya chupa''.
Hatunyoshei kidole cha lawama chapa fulani, ni kuonyesha tu kwamba hili hufanyika kila mahali , kwamba plastiki imekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na imeingia katika maji ,ambayo hutumika sana katika jamii.
Kufikia sasa hakuna ushahidi kwamba utumizi mdogo wa plastiki unaweza kukudhuru, lakini kuelewa athari zake ni muhimu sana katika sayansi.
Uchujaji wa vipande vikubwa katika maji hayo.Haki miliki ya pichaORB MEDIA
Image captionBaada ya kuchuja maji hayo ,vipande vikubwa vyenye rangi ya manjano huonekana kwa urahisi.
Akizungumzia matokeo hayo , Prof Mason alisema: Idadi tunayoona sio janga bali ni jambo la kutia wasiwasi. Wataalam wameambia BBC kwamba watu katika mataifa yanayokuwa ambapo maji ya mfereji huchagfuliwa wanaweza kuendelea kunywa maji kutoka kwa chupa.
Walipoulizwa kuzungumza kuhusu matokeo, kampuni zinazomiliki chapa za chupa hizo zilisisitiza kuwa bidhaa zao zina viwango vya ubora na usalama.
Pia zilizungumza kuhusu ukosefu waheria za kudhibiti vipande vya pal,stiki mbali na ukosefu wa viwango vya kufanya vipimo kama hivuyo.
Mwaka uliopita , Profesa Mason alipata vipande vya plastiki ndani ya maji ya mfereji na watafiti wengine wamepata vipande kama hivyo katika vyakula vya baharini , kwenye pombe, chumvi ya baharini na pia kwenye hewa.
Kazi hii ya hivi karibuni inajiri huku kukiwa na uangalifu wa kimataifa kuhusu plastiki, unaotokana na msururu wa makala ya BBC kwa jina Blue Planet 2 ambapo David Attenborough aliangazia tisho la uchafu wa plastiki katika bahari.
Utafiti huo wa maji ya chupa ulishirikisha ununuzi wa chupa za maji kutoka kampuni 11 tofauti katika mataifa yalio na utumizi wa kiwango cha juu ya maji yanayohifadhiwa katika chupa za plastiki.
Kampuni zinazomiliki chapa hizo ni:
  • Aquafina
  • Dasani
  • Evian
  • Nestle Pure Life
  • San Pellegrino
Chapa za kitaifa zinazoongoza ni:
  • Aqua (Indonesia)
  • Bisleri (India)
  • Epura (Mexico)
  • Gerolsteiner (Germany)
  • Minalba (Brazil)
  • Wahaha (China)
Uchunguzi wa vipande hivyo vya Plastiki ulishirikisha kuongeza rangi kwa jina Nile Red katika kila chupa
Image captionUchunguzi wa vipande hivyo vya Plastiki ulishirikisha kuongeza rangi kwa jina Nile Red katika kila chupa
Ili kuondoa hatari yoyote ya uchafuzi wa maji hayo, maduka ambayo chupa hizo zilinunuliwa yelirekodiwa katika video huku chupa nyengine kutoka Marekani zikiagizwa kupitia mtandaoni.
Uchunguzi wa vipande hivyo vya Plastiki ulishirikisha kuongeza rangi kwa jina Nile Red katika kila chupa, mbinu iliotumiwa hivi karibuni na wanasayansi wa Uingereza kwa ugunduzi wa rahisi wa plastiki katika maji ya baharini.
Utafiti wa awali umebaini vile rangi hiyo husalia katika vipande vya plastiki ndani ya maji na kuvifanya kung'ara vinapowekwa katika mwangaza.
Profesa Mason na wenzake walichuja sampuli zao zenye rangi na kuhesabu vipande vyote vilivyo na ukubwa wa zaidi ya maikroni 100, ikiwa ni sawasawa na upana wa unywele mmoja.
Baadhi ya vipande hivyo , vikiwa vikubwa kuweza kubebwa pekee vilichanganuliwa na miale , kuthibtishwa kuwa plastiki na baadaye kubainika kuwa vipande vya plastiki kwa jina Polymer.
Vipande vidogo vya zaidi ya maikroni 100 hadi vidogo vyenye ukubwa wa maikroni 6.5 vilihesabiwa kwa kutumia mbinu iliotengezwa ili kuhesabu nyota wakati wa usiku.
Uthibitisho wa iwapo vipande hivyo ni vya plastiki haukufanyika lakini profesa Mason anatarajia vipande hivyo ni plastiki.
Kwa kuwa utafiti huo haukupitia njia za kawaida na uchapishaji katika jarida la kisayansi , BBC iliwataka wataalam kutoa matamko yao .
Dr Andrew Mayes, wa chuo kikuu cha East Anglia na mmoja wa waanzilishi wa mbinu hiyo ya Nile Red alituambia kwamba ina ubora wa hali ya juu na kwamba matokeo yake yalikuwa ya kuridhisha.
Michael Walker, mshauri katika serikali ya Uingereza na mwanzilishi wa bodi ya kituo cha ubora wa viwango vya chakula alisema kuwa kazi hiyo iliofanywa kupitia matumizi ya Nile Red ina asili nzuri
Wote wawili walisisitiza kwamba vipande hivyo vya plastiki vilivyo chini ya maikroni 100 havikubainika kuwa plastiki lakini akasema kwamba hakuna chengine chochote kilichotarajiwa kupatikana katika maji hayo isipokuwa vipande vilivyotajwa kuwa plastiki.
Swala kuu ni wapi vipande hivi vya plastiki vinatoka. Ikiangazia idadi ya polypropylene, inayotumika katika vifiniko , huku njia moja ikisema kuwa kitendo cha kufungua chupa kinaweza kuingiza vipande vidogo vya plastiki ndani yake.
David and Prof Mason
Image captionProf Mason takes David Shukman through the results of the study
BBC vilevile iliwasiliana na baadhi ya makampuni yalioshirikishwa na mengi yalijibu kuhusu ugunduzi huo.
Nestle ilituambia kwamba vipimo vyake vya vipande vya plastiki vilianza zaidi ya miaka miwili iliopita na haikugundua uchafu wowote wa kuzidi viwango.
Msemaji wake aliongezea kwamba utafiti wa profesa Mason hatahivyo ulikosa viungo muhimu ili kutoa ukweli lakini akalialika shirika la Orb Media kulinganisha mbinu zilizotumiwa.
Gerolsteiner pia ilisema kwamba imekuwa ikifanyia vipimo maji yake ili kutafuta vipande vya plastiki kwa miaka kadhaa na matokeo yake yamekuwa yakionyesha viwango vya chini vya plastiki .Imesema kuwa haielewi ni vipi Profesa Mason alipata ,matokeo hayo.
Coca-Cola ilisema kuwa ina viwango vya juu vya ubora katika soko la maji na kwamba imekuwa ikitumia mbinu ya 'uchujaji wa hatua baada ya hatua'.
Danone ilisema kuwa haikuweza kutoa maoni yao kuhusu matokeo hayo , mbinu iliotumika lakini ikasema kuwa chupa zake zina viwango vya juu vya kuweka chakula
PepsiCo ilisema kuwa Aquafina ina mikakati ya kuzuia uchafu kama huo katika chakula hatua inayofanya bidhaa zake kuwa salama.

No comments:

Post a Comment