Ukarabati wa jengo hilo uliofanywa na taasisi ya naibu spika huyo ya Tulia Trust, umegharibu Sh40milioni.
Dk Tulia amekabidhi jengo hilo leo Jumatano Machi 7, 2018 katika ziara yake mkoani hapa sambamba na kukagua ukarabati wa mradi huo na kuzungumza na wananchi na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika kituo hicho.
Amesema katika kuunga mkono jitihada za Serikali, taasisi yake imelenga kuboresha huduma muhimu za afya za wajawazito na watoto katika vituo vya afya na zahanati.
"Mkuu wa mkoa (Makalla) nakupongeza kwa jitihada zako mpaka kufikia hatua za mwisho za kusimamia mradi huu sasa ninaomba changamoto za mahitaji madogo yaliyopo yafanyiwe kazi ili huduma za upasuaji zianze kutolewa," amesema.
Kwa upande wake Makalla amesema Serikali imetoa Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa katika Kituo cha Afya Ruanda pamoja na vifaa tiba.
"Naibu Spika ukarabati wa chumba cha upasuaji umekuwa chachu kwa Serikali na sasa imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa katika kituo hiki kwa kweli unatupa moyo sana kama viongozi wa Mkoa," amesema.
Pia, ameagiza halmashauri ya jiji kupitia mapato yake ya ndani kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia baadhi ya mahitaji katika chumba cha upasuaji ili kianze kutoa huduma kwa wananchi
"Natoa wiki mbili ukarabati huu uwe umekamilika na huduma zianze kutolewa mapema iwezekanavyo," amesema.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho, Elioth Sanga amesema wametenga Sh55 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upasuaji.
No comments:
Post a Comment