Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Chama cha Kitaaluma cha Uhusiano na Umma Tanzania (PRST) jijini Dar es Salaam, Jumamosi Desemba 2,2017.
Dk Mwakyembe katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nicolaus William amesema kipaumbele kiwe kwa watakaothibitishwa na bodi ya ithibati ya PRST itakayoundwa.
Amesema ni vyema jamii ikatambua kuwa wanataaluma wa uhusiano wa umma (PR) na wanahabari wanategemeana katika kufikisha taarifa kwa umma.
"Hakuna wanahabari bila wanataaluma wa PR na hakuna wanataaluma wa PR bila wanahabari. PR inachangia asilimia 80 ya habari katika vyombo vya habari," amesema katika taarifa iliyotolewa na chama hicho.
Dk Mwakyembe amekishauri chama cha PRST kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu kuandaa mwongozo wa mafunzo mafupi kwa wanataaluma.
Chama cha PRST kimempa Rais mstaafu Benjamin Mkapa uanachama wa heshima katika uzinduzi huo.
Rais wa PRST, Loth Makuza amemshukuru Mkapa kwa kutoa kipaumbele katika uanzishwaji wa nafasi za wanataaluma wa habari na mawasiliano katika idara za Serikali na taasisi zake mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Uzinduzi wa PRST ulipata ushirikiano kutoka chama cha kimataifa cha uhusiano na umma duniani (IPRA); kingine kama hicho barani Afrika (APRA) na cha nchini Kenya (PRSK).
No comments:
Post a Comment