Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amekutana na wawekezaji wenye nia ya kuzalisha umeme nchini kwa kutumia teknolojia mpya ya sumaku. Alikutana na wawekezaji hao Novemba 13, mwaka huu Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Baada ya kuzungumza na Waziri, wawekezaji hao kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani, walifanya majadiliano na wataalam wa nishati kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Wawekezaji hao walitakiwa kuwasilisha Andiko la Awali (concept note) la Mradi wao ili lipitiwe na kujadiliwa na wataalam husika, kabla ya kuendelea na hatua nyingine stahiki za uwekezaji nchini.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika kikao na wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani (kulia). Kushoto ni maafisa wa Wizara, TANESCO, REA na EWURA.
Mwekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani, Colin Cloete akiwasilisha mapendekezo ya kuzalisha umeme kwa teknolojia mpya ya sumaku, mbele ya Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani na wataalam wa sekta hiyo kutoka Wizarani, TANESCO, REA na EWURA.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani (kushoto), akifafanua jambo kwa wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited, wakati wa kikao baina yao kilichofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akiagana na wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited, waliofika wizarani kuwasilisha mapendekezo ya kuwekeza nchini kwa kuzalisha umeme unaotumia teknolojia mpya ya sumaku.
No comments:
Post a Comment