Monday, November 6

Viongozi ACT- Wazalendo waitikia wito wa polisi


Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Doroth Semu amefika katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Semu amefuatana na Katibu wa Kamati ya Ulinzi ya chama hicho, Mohamed Babu.
Viongozi hao pamoja na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Yeremia Maganja wanatakiwa kufika katika kitengo hicho wakiwakilisha wajumbe wote wa Kamati Kuu ambao walitakiwa kuripoti leo.
Wakati viongozi hao wakiwasili hapo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ameripoti Kituo cha Polisi Chang'ombe jijini Dar es Salaam ambako anatuhumiwa kwa uchochezi.
Baada ya kuripoti kituoni hapo, Zitto ametakiwa kurejea tena Ijumaa Novemba 17,2017.
“Nimeambiwa nirudi wiki ijao siku ya Ijumaa Novemba 17," amesema Zitto.
Kiongozi huyo ameelekea Kamata ambako anatakiwa kuripoti katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha.

No comments:

Post a Comment