Monday, November 6

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WAANZA KUTANGAZA UTALII WA NDANI KUSINI MWA TANZANIA KWA NJIA YA RELI YA TAZARA



alozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. Halfa hiyo ilifanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (kulia) na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG.
Baadhi ya wageni ambao ni wanaumoja wa CAAT wakifuatilia kwa makini. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi akitoa pongezi kwa umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania - CAAT) kwa kuweza kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam. Katika salamu zake Jaji Mihayo aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii ili waweze kujifunza mengi zaidi. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto) akitolea ufafanuzi wa masuala mbali mbali jinsi umoja wao ulivyo na lengo kuu la kuweza kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika.  Halfa hiyo iliyofanyika ijumaa iliyopita TAZARA jijini Dar es Salaam.
 Burudani ya ngoma ikiendelea.  Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akiingia ukumbini.  Vijana wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo (mwenye tai nyekundu) akiwa na Mwenyekiti wa China Alumni Association of Tanzania (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia (kushoto). Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Ronald Phiri wakiwa katika picha ya pamoja na wanaumoja wa CAAT. Hafla hiyo ilifanyika TAZARA jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment