Wednesday, November 1

Tanesco yaendelea na matengenezo Kinyerezi I


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kurekebisha mfumo wa kupokea gesi na usafishaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I inaendelea vizuri.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya uhusiano Tanesco makao makuu kuhusu maendeleo ya matengenezo katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I imesema wataalamu wanaendelea kukagua mitambo ili kuhakikisha usalama zaidi.
Tanesco katika taarifa iliyotolewa leo Jumatano Novemba 1,2017 imewaomba radhi wateja kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
 Pia, imewatahadharisha wananchi wasishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

No comments:

Post a Comment