Singapore imesitisha shughuli zote za biashara na Korea Kaskazini wakati ambapo Umoja wa Mataifa na Marekani wanataka kuiwekewa vikwazo vikali.
Forodha nchini Singapore zilisema kuwa bidhaa za biashara kutoka Korea Kaskazini zilipigwa marufuku kuanzia tarehe 8 Novemba.
Wale watakiuka marufuku hiyo watafungwa kwa hadi miaka miwili.
Marufuku hiyo inachukuliwa baada ya Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kufuadtia jaribio ya sita ya nyuklia.
Singapore ilichukua nafasi ya nane kama mshirika wa kibiashara wa Korea Kaskazini.
Asilimia kubwa ya biashara za korea kaskazini ni pamoja na China, mshirika mkubwa wa kiuchumi wa taifa hilo.
Awamu ya hivi karibu ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa ililenga makampuni na watu binafsi pamoja na makampuni mawili nchini Singapore.
Mwezi Januari mwaka 2016 kampuni moja nchini Singapore ilipigaw faini ya dola 125,000 kwa kusaidia kusafiridsha silaha kutoka nchini Cuba kwenda Korea Kaskazini baada ya mahakama kupata kuwa kampuni ya Chinpo wa usafiri wa baharini ilikiuka azimio la Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment