Friday, November 17

Mungo Man: Mabaki ya kale zaidi ya binadamu yapelekwa nyumbani Australia

An Aboriginal elder prepares to welcome the return of the remains of Mungo ManHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUchunguzi ulionyesha kuwa mabaki hayo yalikuwa ni ya miaka 42,000 iliyopita,
Kwa miongo kadhaa mabaki ya binadamu ya kale zaidi nchini Australia ya mtu ambaye alifariki karibu miaka 42,000 iliyopita yamekuwa yakihifadhiwa katika chuo kikuu na kwenye makavazi.
Lakini leo Ijumaa, mabaki hayo yanayojulikana kama Mungo Man, yalisafirishwa nyumbani kwao eneo la New South Wales na kupewa heshima katika sherehe.
Ilifikisha mwisho wa kampeni na watu wa asili nchini Australia ya kutaka Mungo Man kurejeshwa nyumbani kwao.
Kugunduliwa kwa mabaki hayo mwaka 1974 kulichangia kuandikwa upya historia ya Australia.

Mungo Man ni nani?

Mabaki hayo yakifukuliwa na mwanajiolojia Jim Bowler kutoka na sakafu ya lililokuwa ziwa kwneye mbuga ya kitaifa ya Mungo karibu kilomita 750 magharibi mwa Sydney na kutaja kuwa ugunduzi mkubwa.
A casket holding the remains of Mungo ManHaki miliki ya pichaNSW OFFICE OF ENVIRONMENT & HERITAGE
Image captionUchunguzi ulionyesha kuwa mabaki hayo yalikuwa ni ya miaka 42,000 iliyopita,
Mabaki ya Mungo Man kisha yakapelekwa katika chuo kikuu cha Australia kwenda kufanyiwa utafiti.
Uchunguzi ulionyesha kuwa mabaki hayo yalikuwa ni ya miaka 42,000 iliyopita, na ndiyo ya kale zaidi ya binadamu nchini Ausralia.
Wanasayansi wanasema kuwa Mungo Man alikuwa mwindaji ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 50.

Safari ya kurudi nyumbani

Jamii za asili kutoka eneo hilo zimeomba kwa siku nyingi kurejeshwa kwa mabaki hayo zikisema kuwa kuondolewa kwao kuliwaletea huzuni kubwa.
Waakilishj kutoka jamii za Mutthi Mutthi, Ngiyampaa na Paakantji/Barkandji walifanya sherehe leo Ijumaa.
Indigenous dancers welcome Mungo Man remains back to countryHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaakilishj kutoka jamii za Mutthi Mutthi, Ngiyampaa na Paakantji/Barkandji walifanya sherehe leo Ijumaa.

No comments:

Post a Comment