Monday, November 13

Saad Hariri: Nitarudi Lebanon siku chache zinazokuja

Lebanese watch an interview with Saad Hariri at a coffee shop in BeirutHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKujiuzuku kwa Hariri kulizua msukosuko nchini Lebanon
Waziri mkuu wa Lebabon Saad Hariri anasema kuwa atarudi nyumbani siku chache zinazokuja kutangaza rasmi kujiuzulu kwake.
Bw. Hairi aliongea na runinga ya Future kutoka mjini Riyadh, yakiwa ndiyo matashi yake ya kwanza tangu atangaze wiki iliyopita kuwa alikuwa anajiuzulu.
Washirika wakae wanasema kuwa anashikwa mateka lakini Bw. Hariri anakana hayo.
Amelilaumu kumndi linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah kuwa sababu ya kujiuzulu kwake akisema alihofia usalama wake na wa familia yake.
Hariri ambaye na kiongozi wa Sunni na mfanyabiashara, aliteuliwa kuunda serikali ya Lebanon mwezi Novemba mwaka 2016.
Posters depicting Lebanon's Prime Minister Saad al-Hariri, who has resigned from his post, are seen in Beirut, Lebanon, on 10 November 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMabango ya kumuunga mkono Hariri mjini Beirut
"Nimejiuzulu. Ninaenda Lebanon hivi karibuni na nitajiuzulu kuambatana na kabika," alisema wakati wa mahojiano ya televisheni,.
Kupitia hotuba iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni kutoka mji wa Riyadh Bw. Hariri aliilaumu Iran na Hezbollah kwa kudhibiti Lebanon na kulivurujga eneo lote hio.
Bw. Hariri alisema kuwa ikiwa atabatilisha uamuzi wake wa kujiuzulu, basi Hezbolla ni lazima iheshimu sera na kukaa nje ya mizozo ya kimaeneo.
Iran na Hezbollah wameilaumu Saudi Arabia kwa kumshikilia Bw. Hariri Mateka.
Lakini Bw. Hariri alisema kwa yuko huru kusafri anavyotaka akiwa nchini humo.

No comments:

Post a Comment