Baadhi ya majeshi ya polisi makubwa kuliko yote katika nchi za Afrika, ambayo tayari sifa yao imeharibika, yanaonyesha kujihusisha zaidi na kupiga raia.
Kwa mujibu wa Rikodi iliyotayarishwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Sayansi ya Kimataifa na Taasisi ya Uchumi na Amani, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi hizo mbili ambazo ziko katika nchi tano zenye wastani wa chini kabisa wa idadi ya maafisa wa polisi duniani, zinakabiliwa na masuala yanayofanana na hali ya ulinzi Nigeria.
Kwa mwaka 2016, vurugu za kisiasa zilipoongezeka, Polisi Kenya walikabiliwa na madai ya kufanya mauaji ya kinyama kuliko sehemu nyingine zozote Afrika.
Jeshi la polisi DRC linajukumu la kudhibiti maandamano kadhaa ambayo yameenea katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo baada ya uamuzi wa Rais Joseph Kabila kusema atabakia kwenye madaraka.
Kenya na DRC wana maafisa wa polisi 99 na 100 kwa kila raia 100,000. Uganda kwa kiasi fulani inaunafuu zaidi kwa kuwa na maafisa wa polisi 110 kwa raia 100,000.
Mwaka jana, Serikali katika utafiti wake iligundua kuwa wananchi wa Uganda wanaamini kuwa jeshi la polisi nchini Uganda la ufisadi wa hali ya juu.
Kati ya nchi 127 zilizotathminiwa katika Rikodi ya Dunia ya Vyombo vya Usalama vya ndani na Polisi, Jeshi la Polisi Nigeria linaongoza kwa upigaji wa raia, ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya na Uganda ambazo ndiyo nchi nne za mwisho katika orodha hiyo.
Rikodi hiyo, iliyotayarishwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Sayansi ya Kimataifa na Taasisi ya Uchumi na Amani, inayoangalia ni kiwango gani cha rasilmali kila taifa linatenga kwa ajili ya usalama wa ndani, iwapo rasilmali hizo zinatumika kwa ufanisi na iwapo wananchi wanalipenda jeshi lao la polisi.
Rikodi hiyo pia inatathmini hali ya hatari inayo vikabili vyombo vya usalama vya ndani katika kila nchi.
Kati ya maeneo yote, Amerika Kaskazini na Ulaya zinaonyesha majeshi ya polisi katika nchi hizo yalivyokuwa na uwezo wa hali ya juu katika kukabiliana na masuala ya usalama wa ndani.
Lakini wakati huohuo nchi zilizoko kusini mwa sahara zimeonyesha kuwa na uwezo wa chini katika masuala ya kiusalama kama wasimamizi wa usalama katika eneo hilo wakiwa na upungufu wa rasilmali na kupata shinikizo la mashambulizi kutoka kwa vikundi vya kigaidi na waasi. “Rikodi ya Nigeria inaonyesha ni katika nchi 10 za mwisho katika vigezo vyote vilivyotumika kuwatathmini.
Nigeria ina maafisa wa polisi 219 kwa kila raia 100,000—chini ya kiwango cha kati kinachokubalika cha polisi 300 na nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa jJangwa la Sahara zinawastani wa polisi 268, kwa mujibu wa ripoti hiyo. Taasisi za usalama binafsi haziwezi kuziba mwanya huo uliopo kwa kuwa na walinzi 71 kwa Wananchi 100,000—moja ya nchi tano zilizopata tathmini ya chini kabisa ukilinganisha na nchi zote duniani.
No comments:
Post a Comment