Nyota wa filamu Portia de Rossi amemtuhumu nyota mwenza wa filamu na mtayarishaji Steven Seagal kwa unyanyasaji wa kinjinsia.
Nyota huyo wa filamu ya The Arrested Development , ambaye ameolewa na mtangazaji wa Marekani Ellen DeGeneres, alitoa madai hayo katika chapisho la ujumbe wa Twitter siku ya Jumatano usiku.
Anadai wakati wa ukaguzi wa kuwaajiri wale watakaoigiza katika filamu, bwana Seagl alimwambia umuhimu wa wao wawili kulala pamoja kabla ya kufungua zipu ya suruali ndefu aliyokuwa amevaa.
Meneja wa bwana Seagal aliambia BBC kwamba nyota huyo hana tamko la kutoa.
Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 65 anajulikana kwa uigizaji wake miaka 1980 na 1990, ikiwemo filamu ya Under Siege na Flight of Fury.
Alipewa uraia wa Urusi na rais wa taifa hilo Vladmir Putin 2016.
Wanawake wengine kadhaa wamejitokeza kumshutumu bwana Seagal kwa kuwa na tabia mbaya akiwemo nyota wa filamu ya Good Wife Julianna Margulies na mwanamitindo Jenny McCarthy.
Ni nyota wa hivi karibuni wa Hollywood kushutumiwa na maswala ya unyanyasaji wa kijinsia baada ya wanawake kujitokeza dhidi ya mtayarishaji wa filamu Harvey Weinstein.
Harvey Weinstein hatahivyo amekana madai yote ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake.
Katika chapisho la ujumbe wa Twitter, bi de Rossi alisema malalamishi yake kuhusu tabia za bwana Seagal yalipuuziliwa mbali wakati huo na ajenti wake.
Hakutaja ni filamu gani ambayo alitarajiwa kuigiza na ni mwaka gani kisa hicho kilitokea.
Nyota huyo mwenye uraia wa Australia na Marekani ameolewa na mtangazaji wa runinga Ellen DeGeneres kwa miaka tisa sasa.
Bi DeGeneres alisambaza ujumbe wa twitter wa bi de Rossi kwa wafuasi wake milioni 75 siku ya Alhamisi ikiwa na maneno: Nampenda mke wangu.
No comments:
Post a Comment