Friday, November 10

Adanganya alitekwa nyara ili kumuona mpenzi wake Ufaransa

Msako mkubwa uliohusisha wanajeshi 50 na helikopta moja ulifanywaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMsako mkubwa uliohusisha wanajeshi 50 na helikopta moja ulifanywa
Mwanamke mmoja aliyejidai ametekwa nyara ili kumuona mpenziwe amehukumiwa kifungo cha miezi sita na mahakama moja ya Ufaransa.
Sandy Gaillard mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mwanaharakati wa chama cha mrengo wa kulia cha National Front aliwafanya maafisa wa polisi kuanzisha msako mkubwa uliohusisha wanajeshi 50 na helikopta moja ,mahakama iliambiwa.
Alitalakiana na mumewe na kuanza kuishi na mpenziwe lakini akafanya njama hiyo ili kumuona mwanamume wa tatu.
Alipigwa faini ya €5,000 (£4,400; $5,800) na kuagizwa kumuona daktari wa kushughulikia maswala ya akili.
Mpenziwe Gaillard aliwaelezea maafisa wa polisi mnamo mwezi Julai wakati alipomtumia ujumbe kwamba alikuwa ametekwa nyara katika buti ya gari nyeusi , mahakama hiyo iliopo mji wa kusini wa Mende iliambiwa.
Na kufuatia usakaji wa saa 24 alijitokeza bila kuonyesha ishara zozote za maumivu ama vitisho na kusema kuwa waliomteka waliamua kumwachilia.
Taarifa yake ilikosa mwelekeo na mamlaka ikawa na wasiwasi.
Na alipoendelea kuhojiwa na maafisa wa polisi alikiri kwamba alidanganya ili kukutana na mpenziwe katika eneo la Le Puy-en-Velay, mahakama iliambiwa.
Anasema kuwa mpenzi wake mpya hakushiriki katika udanganyifu huo.

No comments:

Post a Comment