Rais wa Zimbabwe Robert Kugabe amemlaumu makamu wake wa rais aliyefutwa, Emmerson Mnangawa kuwa alikuwa akiwauliza waganga ili kujua ni lini yeye Mugabe 93, angekufa, wakati akipanga kuchukua madaraka, gazeti la serikali la Herald lilisema.
Bwana Mnangawa kwanza alisambaza uvumi kuwa rais alipanga kustaafu mwezi Machi lakini baada ya kugundua kuwa hilo halikufanyika, alianza kuwauliza waganga kuhusu ni lini nitakufa, Bw Mugabe alisema.
Wakati mmoja aliambiwa kuwa atakufa kabla ya mimi.
- Rais Robert Mugabe amemfuta kazi Makamu wa Rais
- Bi Grace Mugabe ataka makamu wa rais afutwe kazi
- Rais wa Cameroon aadhimisha miaka 35 uongozini
Akiwahutubia maelfu ya wafuazi kwenye mji mkuu Hararare, Bw Mugabe alisema kuwa Mnangawa alikosa maadili na alijaribu kuanzisha uasi kwenye chama tawala cha Zanu-PF.
Siku ya Jumatatu Mugabe alimfuta Mnangawa, mshirika wa karibu wake tangu vita vya uhuru vya miaka ya sabini, katika kile wadadisi wanasema kuwa ni njia ya kumwezesha mke wake Grace kuchukua madaraka wakati wakakufa au kustaafu.
Bw. Mugabe anatarajiwa kumteua Grace kuwa makamu wa Rais.
Grace amekuwa akitoa wito wa kutaka kufukuzwa Mnangawa kutoka chama cha Zanu-PF, ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980.
No comments:
Post a Comment