Thursday, November 9

Marekani yaongezewa masharti Cuba

Miongoni mwa Hotel ambazo Wamarekani wamepigwa marufuku kufikia nchini CubaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiongoni mwa Hotel ambazo Wamarekani wamepigwa marufuku kufikia nchini Cuba
Serikali ya Marekani imetangaza masharti mapya yenye nguvu zaidi yatakayoweka ugumu wa Wamarekani kutembelea Cuba na kufanya biashara nchini humo.
Ikulu ya Marekani imesema sheria mpya hizo zinalenga kuzuia wanajeshi na wana Usalama kunufaika na utalii na biashara kutoka Marekani.
Masharti hayo ambayo yanahusisha marufuku juu ya Wamarekani kutumia makampuni 180 ikiwemo hoteli za serikali na maduka yanayohudumia wanajeshi.
Masharti hayo pia ni pamoja na raia wa Marekani wanapotaka kusafiri nchini Cuba wanapaswa kuthibitisha kwenye kampuni moja ya nchi hiyo inayohusika na masuala ya safari.

No comments:

Post a Comment