Wednesday, November 29

Kwa nini mkewe mwanamfalme Harry hataitwa bintimfalme Meghan

Mwanamfalme Harry na mchumba wake Meghan MarkleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamfalme Harry na mchumba wake Meghan Markle
Kwa nini Meghan Markle hataitwa kwa jina bintimfalme Meghan wakati atakapofunga ndoa na mwanamfalme Harry mwaka ujao?
Jibu ni kwamba kulingana na viwango vya itafaki ya ufalme wa Uingereza, nyota huyo wa zamani wa Hollywood hana damu ya ufalme.
Hio ndio sababu hawezi kuitwa mwanamfalme Meghan.
Sheria hiyo inamaanisha kwamba Meghan atalazimika kufuata mifano ya dada zake wa kambo.
Catherine Middleton wakati wa ndoa yakeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCatherine Middleton wakati wa ndoa yake
Ni damu ya kifalme inayoamua jina la mwanamfalme wa kikeHaki miliki ya pichaPA
Image captionNi damu ya kifalme inayoamua jina la mwanamfalme wa kike
Wakati Catherine Middleton na mwanamfalme William walipofunga ndoa walitangazwa kuwa mume na mkewe, 2011, na tayari Kate akachukua jina la bintimfalme Williams wa Wales.
Uwezekano mkubwa ni kwamba mchumba huyo mpya atatumia jina la bintimfalme Harry wa Wales.
Rasmi, tunaweza kusahau mwanamfalme Kate na tunaweza kusahau mwanamfalme Meg.
Sababu ni kwamba Catherine Middleton hakuwa na damu ya kifalme na kwamba mfano huo pia utamkabili Meghan Markle.
Kuwa na damu ya kifalme kunamaanisha kwamba dadake malkia Margaret alitakikana kujiita mwanamfalme Margaret.
Vilevile mwana wa kike wa malkia ni mwanamfalme Anne na wajukuu wake ni bintimfalme Beatrice na Eugine.
Damu ya kifalme inawafanya kuwa wafalme.
Lakini Sarah Furguson hakuweza kuwa bintimfalme Sarah na Sophie Rhys-Jones, mkewe mwanamfalme Edward sio bintimfalme Sophie.
Mwanamfalme Diana wa Wales
Mwanamfalme Diana wa Wales
Image captionMwanamfalme Diana wa Wales
Sheria hiyo pia inaonyesha kuwa Diana Spencer hakuitwa mwanamfalme Diana.
Alikuwa akiitwa mwanamfalme Diana wa Wales na baada ya kutalakiana na mwanamfalme Charles, aliitwa Diana, mwanamfalme wa Wales.

No comments:

Post a Comment