Tuesday, November 7

Kimbunga chaua watu 49 Vietnam


Mbwa wakiwa katika duka la vinywaji baada ya kukimbia mafuriko nchini Vietnam
Kimbunga chenye nguvu kimeikumba pwani ya Vietnam na kuuwa watu 49, na zaidi ya dazeni ya watu hawajulikani waliko pamoja na kusababisha madhara makubwa katika eneo hilo.
Watu 19 hawajapatikana, wakiwemo mabaharia tisa wa meli kadhaa za mizigo ambazo zilizama nje ya pwani ya jimbo la Khanh Hoa, Mamlaka ya Kusimamia Maafa Vietnam imesema katika tamko lake Jumatatu.
Mafuriko yameripotiwa maeneo mengi na zaidi ya makazi 116,000 yameagamizwa au kuharibiwa, tamko hilo limesema.
Kimbunga hicho kinachojulikana kama Damrey kimeikumba Vietnam Jumamosi kimekwisha malizika, lakini ofisi ya wakala wa maafa imesema mafuriko yanaweza kufikia hali mbaya zaidi kama utabiri wa mvua hizo unavyoonyesha katika eneo hilo.
Mji mkuu wa Da Nang, ambao mkutano wa Ushirikiano wa Uchumi wa Nchi za Asia (APEC) unaohudhuriwa na viongozi wa ulimwengu kutoka Novemba 8-10, pia umeshuhudia mvua kubwa.
Viongozi wa nchi 21 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, akiwemo Rais Donald Trump, Rais wa China Xi Jinping, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, na Rais wa Russia Vladimir Putin.

No comments:

Post a Comment