VIJIMAMBO na BMJ Muriithi Mbwa mmoja nchini Marekani, ameweka rekodi ya kuwa na ulimi mrefu kuliko mbwa mwingine yeyote duniani. Moch Richert, ambaye anajulikana kwa jina la utani kama MO, ana umri wa miaka minane na anatokea mjini Sioux Falls, katika jimbo la South Dakota.
Kitabu cha Guiness Book of world records kimemuorodhesha mbwa huyo kama aliyeweka rekodi mpya kwa kuwa na ulimi wenye urefu wa ajabu.
Mwenye mbwa huyo, Carla Richert, amewaambia waandishi wa habari kwamba;
"Ulimi wake una urefu wa inch 7.3 ambazo ni kama centimita 18.58," alisema Richert.
Moch sasa amechukua nafasi iliyoshikiliwa na mbwa aitwaye Puggy ambaye alikuwa amemshinda mbwa aliyepata umaarufu mkubwa Zaidi duniani Brandy the Boxer takriban miaka 10 iliyopita.
Je wewe msikilizaji, iwapo una mbwa, una habari ulimi wake una urefu kiasi gani?
Tafakari hayo.
Ukitafakari hayo, hebu tuone mengine yaliyojiri katika maeneo mengine duniani.
Tunasafiri moja kwa moja hadi kaunti ya Migori nchini Kenya. Kulikoni?
Wakazi wanalalamika kuwa miili ya watu waliokufa imekuwa ikifukuliwa na wanyama kwa sababu ya kuzikwa kwenye makaburi ambayo hayana urefu wa kutosha.
Amini usiamini msikilizaji, watoto wengi wamekuwa wakilalamika kwamba awamekuwa wakipata mili barabarani ambayo imevutwa na baadhi ya wanyama katika eneo hilo. Kulikoni?
No comments:
Post a Comment