Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara mama yake na dada yake, wote wamekana mashtaka dhidi yao yanayohusu kuchochea uasi, walipofikishwa kwenye mahakama ya mjini Kigali.
Hata hivyo jaji alihairisha kesi hiyo baada ya mama yake Rwigara, Adeline Rwigara, ambaye anakabiliwa na mashtaka tofauti kusema anataka wakili wake kuweza kumuakilisha.
Diane Rwigara tayari anakabiliwa na mashtaka ya kubuni stakabadhi bandia, alizopanga kutumia kuwania urais wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti.
- Polisi Rwanda wafanya msako nyumba ya aliyetaka kuwania urais
- Mkosoaji wa Kagame afunguliwa mashtaka ya kuchochea uasi
- Mwanamke kuwania urais nchini Rwanda
Alizuiwa kugombea uchaguzi huo ambao ulishindwa na Rais Paul Kagame.
Mwanaharakati huyo maarufu wa masuala wa wanawake na mkosoaji mkubwa wa Bw. Kagame, alisema kuwa mashtaka dhidi yao yamechochewa kisiasa.
Wote hao bado wako katika kuzuizi cha polisi.
No comments:
Post a Comment