Tuesday, October 10

Trump aomba ufadhili wa ujenzi wa ukuta na kufukuzwa kwa wahamiaji

Protesters hold up signs during a demonstration against US President Donald Trump during a rally in support of the Deferred Action for Childhood Arrivals (Daca) in New York, 5 OctoberHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDreamer supporters rallied outside Trump Tower in New York last week
Ikulu ya Marekani imejumuisha makubaliano yoyote mapya kuhusu wahamiaji wadogo wasio na vibali vya uhamiaji na kuwazuia wahamiaji wasio halali, pamoja na ujenzi wa ukuta mpya kati ya mpaka wake Mexico.
Rais wa Marekani Donald Trump anaomba ufadhili kwa ujenzi wa ukuta, kufukuzwa haraka watu kutoka Marekani na kuajiriwa maefu ya maafisa wapya wa uhamiaji.
Mwezi ulioita alifuta mpango wa Obama uliofahamika kama "Dreamer" ambao ulikuwa unawalinda wahamiaji 690,000.
Lakini wanademokrat wenye ushawishi katika bunge wamekataa mapendekezo hayo mapya.
Mwezi uliopita Bw. Trump aliliambia bunge la Congress lililo na warepublican wengi kuwa lina miezi sita kukubaliana kuhusu sheria ya kuwasaidia Dreamers.

Dreamers ni akina nani?

Hawa ni vijana ambao walipelekwa nchini Marekani kinyume cha sheria kama watoto na hivyo wanakabiliwa na hatua ya kufuzwa kutoka nchini humo.
Chini ya sera za Obama, vijana hao walikuwa na uwezo wa kuomba vibali vya kufanya kazi na kusoma, lakini wakosoaji wanasema kuwa mpango huo ni sawa na kuwapa kinga wahamiaji haramu.
Tangu mpango huo uanze kutekelekwa karibu hali ya wahamiaji 100,000 imebadilika kati ya karibu wahamiaji 690,000.

No comments:

Post a Comment