Tuesday, October 10

Tanzania kunufaika na wataalamu wa Afya wa Cuba

Jopo la madaktari bingwa 16 kutoka nchini Cuba
Image captionJopo la madaktari bingwa 16 kutoka nchini Cuba
Jopo la madaktari bingwa 16 kutoka nchini Cuba hivi sasa watafanya kazi katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Lengo la kuwepo kwa madaktari hao ni kushirikiana katika kutoa uzoefu hivyo kusaidia katika utoaji wa huduma za afya hospitali hapo na vilevile kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Prof Lawrence Museru amesema kuanzia leo, madaktari hao waliobobea katika fani mbalimbali watafanya kazi zaidi katika kitengo cha wagonjwa mahututi, na watakuwa nchini humo kwa muda wa miaka miwili .
Prof Museru amesema, miongoni mwa madaktari hao, kumi kati yao ni wataalamu wa mambo ya uuguzi, wawili ni wataalamu wa ganzi, huku wawili wakiwa madaktari wa wodi ya dharura(ICU) na wengine ni wa upasuaji wa macho au kufanyiwa marekebisho ya muonekano wa macho.
muhimbili
Image captionKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dr .Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari
Akiongea na waandishi wa habari kipindi akiwapokea madaktari hao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dr .Mpoki Ulisubisya amesema Tanzania ina mengi ya kujifunza kutoka Cuba.
"Cuba ni nchi ya kwanza kutokomeza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, hivyo tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa madaktari wa Cuba," alisema katibu mkuu huyo kutoka Wizarani.
"Huduma muhimu ya afya bado inakuwa nchini Tanzania. Kuwepo kwa mabingwa hawa, kutainua kiwango cha utendaji wa madaktari wetu. Hivyo wamekuja kwa wakati muafaka," ameongeza kusema.
Nchini Tanzania, uwiano kati a daktari na mgonjwa ni 1:25,000 wagonjwa, hio ni kwa mujibu wa Shirika la Afa Duniani-WHO.

No comments:

Post a Comment