Tuesday, October 10

TAFCA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI


Na Sixmund Begashe.

Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli kwa mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wake ambao amewaapisha Ikulu Dar es Salaam jana.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa TAFCA bw Adrian Nyangamalle kupitia mtandao wa shirikisho hili kubwa hapa nchini ambapo pia bw Nyangamalle alichukuwa nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe (Mb) kwa kubakizwa kwenye wizara yake ya awali pia Mh Juliana Daniel Shonza (Mb) kuwa Naibu Waziri mpya wa wizara hiyo.

“Kwa namna ya pekee tunampongeza Mhe. Juliana Daniel Shonza (Mb) kwa kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na vilele tunampongeza Mhe. Dr Harrison G. Mwakyembe (Mb) kwa kuendelea kuwa Waziri katika Wizara hii, kuendelea kwake kunaonesha namna Mhe. Rais wetu Dr John Joseph Pombe Magufuli alivyo kuwa na imani nae nasi tunatafasiri hivyo kuwa ni ishara ya utumishi wake uliotukuka “ Alisema Bw Adrian.

Bw.Nyangamalle ameongeza kuwa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania ambalo analisimamia litaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa Mawaziri na viongozi wote wa Wizara hiyo katika kuhakikisha wanatimiza malengo ya kuinua Sanaa na Wasani hususani wale wanao jishughulisha na Sanaa za Ufundi nchini ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.
Pichani ni Rais wa TAFCA Bw Adrian Nyangamale

No comments:

Post a Comment