Seneta wa Chama cha Republican nchini Marekani, Jeff Flake, amesema hatogombea nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka 2018.
Amesema nafasi yake inaweza isiwepo katika chama hicho.
Katika hotuba kali inayokosoa utawala wa rais Trump, seneta huyo wa jimbo la Arizona amesema katu hatoacha kusema.
Ameongeza kusema kuwa siasa za Marekani zimekuwa za kutojali, na tabia ya kujishusha hadhi kutoka ikulu ya Marekani.
Lakini amesema, desturi ya kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake katu isionekane kama jambo la kawaida.
- Trump azidi kukosolewa
- Trump lawamani kuhusu matokeo Marekani
- Trump amfuta kazi muendesha mashtaka wa Manhattan
Mwanzoni, rais Trump alilaumiwa na seneta mwengine wa Republican, Bob Corker, ambae alimweleza rais huyo kama rais ambae sio mwaminifu.
Msemaji kutoka ikulu ya White House Sarah Sanders amesema "huenda ni hatua nzuri" Bwana Flake anajiuzulu, akiashiria kwamba hatoshinda kuchaguliwa tena.
No comments:
Post a Comment