“Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na naamini tutashinda,” amesema.
Nyumba hiyo imebomolewa Ijumaa ya Septemba 29 na Wakala wa Barabara(Tanroads) kutokana na kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya yenye upana wa mita 121.5.
Ubomaji wa nyumba hiyo unaenda sambamba na ubomoaji wa nyumba zaidi ya 1,000 zilizo ndani ya hifadhi hiyo ya barabara.
Profesa J ameelezea kubomolewa kwa nyumba yake hiyo katika ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika “Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara tarehe 29/9/ 2017,”umesomoka ujumbe huo.
Ameandika kuwa akiwa katika majukumu jimboni Mikumi saa kumi mbili jioni, alitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na greda mbili na magari mawili ya polisi yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yake.
“(Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads
wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani,”
“Saa kumi na mbili jioni haukuwa muda wa kazi na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu, limenisikitisha,”
“Nimejifunza kumtegemea na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani.”
No comments:
Post a Comment