Polisi wanajaribu kugundua sababu ya ufyatuaji mkubw wa risasi uliosababisha vifo vya watu 59 na kuwajehi wengine 527 kwenye warsha moja huko Las Vegas.
Mtu mwenye silaha Stephen Paddock, 64, alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa warsha moja ya mziki Jumapili usiku.
Polisi walipata bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli na zingine 19 na vilipuzi nyumbani kwake huko Nevada.
Lakini hadi sasa hakuna sababu ya hatua hiyo yake iliyoibuka.
Wachunguzi hawajapata uhusiano wowote na ugaidi licha ya kundi la Islamic State kudai kuhusika.
Baadhi ya wachunguzi wamedai mtu huyo kuwa na matatizo kisaikolojia lakini hio bado halijathibitishwa.
Mtu huyo hakuwa anafahamika kwa polisi.
Stephen Paddock aliishi katika jamii ya watu wazima kwenye mji mdogo wa Mesquite kaskazini mashariki mwa Las Vegas
Aliripotiwa kuishi na mwanamke kwa jina Marilou Danley ambaye kwa sasa yuko nchini Japan na polis wanasema kuwa yaonekana hakuhusika
No comments:
Post a Comment