Tuesday, October 3

Matayarisho ya taarifa nzito kuhusu mazingira

Unapenda mazingira? Jee unataka kufanikiwa kuwa mwandishi wa habari makini wa mazingira? Mwandishi wa Idhaa ya Dunia ya BBC (BBC World Service) anatoa ushauri namna ya kuzipata habari mpya kuhusu mazingira, kuziongeza maelezo na kuvutia watumizi wa mitandao ya kijamii.

Kwa waandishi wa habari kuhusu mazingira kama Navin Singh Khadka wa BBC World Service, ni muhimu siyo kuandika matukio tu bali piya muelekeo, sababu na sayansi kuhusu taarifa yenyewe.
Navin anatoa muhtasari:
  • Kwanini taarifa kuhusu mazingira ni muhimu
  • Majukumu ya waandishi wa habari za mazingira
  • Namna ya kuvutia wengi
  • Namna ya kujitokeza kama mwandishi  kuhusu mazingira
“Kitu muhimu sana ni kuziona hizo habari. Utaweza kufanya hivyo ukitembelea maeneo husika”  – Navin Singh Khadka
Navin  anasisitiza umuhimu wa kufikia eneo ili kupata asili ya taarifa na wakati wote kuonesha kwenye Facebook na Twitter picha na matamshi na majibu kuhusu habari mpya.
Navin amekulia Nepal na awali alifanya kazi katika idhaa ya Nepali ya BBC -  the BBC's Nepali Service. Navin ni mwanataaluma mteuliwa wa kimataifa wa uandishi wa habari unaohusu mabadiliko ya hali ya hewa.  

No comments:

Post a Comment