Taarifa ambazo zimetolewa na Meneja mkuu wa Mlimani City, Pastory Mrosso zinasema sababu za kufungwa huko ni kutokana na kudaiwa kodi ya miezi mitatu mfululizo ambayo ni takriban Sh300 milioni.
Sababu nyingine, Mrosso amesema ni kupungua kwa ufanisi mpaka chini ya wastani. “Bidhaa wanazostahili kuwa nazo hazikidhi mahitaji. Zimepungua kuliko viwango vinavyokubalika,” amesema Pastory.
Nakumatt inaungana na maduka ya Uchumi kutoka nchini Kenya ambayo yanakabiliwa na ukata kiasi cha kushindwa kujiendesha. Serikali ya Kenya imelazimika kuingilia kati madeni ya Uchumi na kuahidi kuwalipa wasambazaji walioikopesha Uchumi.
Kuyumba kwa Nakumatt kulianza Mei, ilipotangaza kuyafunga matawi yake yote yanayojiendesha kwa hasara hasa Tanzania na Uganda. Wiki iliyopita, imelifunga tawi lake kubwa la Bamburi lililopo Mombasa, Kenya pamoja na Lungalunga iliyopo jijini Nairobi.
Hata hivyo, ndani ya miezi miwili iliyopita, Nakumatt imeyafunga matawi yake matatu jijini Nairobi ambayo ni Thika Road Mall, NextGen na Westlands.
Taarifa zinasema Nakumatt inapanga kupunguza gharama za uendeshaji kwa walau Sh30 bilioni kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment