Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Wazalendo ACT , Samson Mwigamba amejiuzulu wadhifa wake leo Oktoba 16.
Mwigamba amesema kwamba ameamua akae pembeni ili awe na nafasi nzuri ya kuwahoji vizuri viongozi wa chama chake hivyo ameamua kubaki kuwa mwanachama mwema.
"Nimeamua kukaa kando kwani tumekuwa hatukubaliani baadhi ya mambo ndani ya Chama hasa Kiongozi wetu," amesema Mwigamba na kuongeza:
"Wacha nikae pembeni niwe mwanachama ili niwe na nafasi ya kuwahoji vizuri viongozi wetu masuala mbalimbali na nitabaki kuwa mwanachama mwema’’ amesema
Katika barua yake ya kujizulu Mwigamba ambayo amemuandikia kiongozi wa chama hicho amesema kwamba ‘’Mnamo Aprili 25,2016 nilipokuwa nang’atuka ukatibu mkuu, nilipotoa nasaha zangu mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama nilisema ,”salama ya chama chetu ni kubaki kwenye misingi ya uanzishwaji wake’’
Anasema haikuwa bahati mbaya bali alimaanisha kwasababu alishaanza kuona mwelekeo wa baadhi ya viongozi wa chama wanachepuka nje ya chama.
Amesema baada ya hapo amekuwa akiwalalamikia sana viongozi ambao wameacha misingi na mambo ya msingi yaliyowafanya waanzishe chama.
Amesema kwamba ‘’kwa sababu hali hiyo inazidi kuongezeka jambo ambalo mimi binafsi naamini ndiyo sababu hasa Profesa Kitila Mkumbo akaamua kujivua uanachama.
Hivyo baada ya kutafakari sana nimeamua kujitenga na uongozi wa sasa wa chama ili niwe huru kuwahoji nyinyi viongozi kwa kauli ,matendo na maamuzi yenu ndani ya chama nikiwa mwanachama wa kawaida.
No comments:
Post a Comment