Wednesday, October 4

Mtoto ateketeza mdogo wake ndani ya nyumba


Watu watano wamekufa wilayani hapa mkoani Kagera katika matukio tofauti, likiwamo la mtoto wa miaka miwili kuteketea ndani ya nyumba baada ya ndugu yake kuwasha kiberiti.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Asteria Lomwadi alisema alikwenda kuchota maji juzi mchana, mtoto wake wa miaka minne aliwasha kiberiti na kuteketeza nyumba hiyo, Kisiwa cha Bumbile.
Katika tukio lingine, Baraka Ntezimana (30) aliuawa usiku wa kuamkia Oktoba 2 Kijiji cha Kyota, Kata ya Kimwani wilayani Muleba kwa wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi aliwataja wengine kuwa ni Morice Mtoni (59) mkazi wa Bumbile; Jackson Domician (9) wa Kijiji cha Buyaga na Muchunguzi Silidon (29) wa Kijiji cha Bugasha, kisiwani Bumbile.

No comments:

Post a Comment