Wednesday, October 11

Miss Universe Tanzania awageukia wadau wa michezo


Dar es Salaam. Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk ameiomba jamii kusaidia watoto wenye ugonjwa wa midomo sungura ili wapate matibabu yanayofaa.
Jihan alisema hayo wa maadhimisho ya "Smile Day" katika Hospitali ya CCBRT ya jijini kwa kushirikiana Taasisi ya Smile Train Africa inayoshughulikia tatizo la mdomo sungura.
Jihan ambaye ni balozi wa shirika hilo, alisema kuwa jamii inatakiwa kuwakubali na kushirikiana katika kutatua tatizo hilo ambao linawaathiri sana watoto wadogo.
Alisema kuwa Taasisi ya Smile Train Africa linatambua tatizo la ugonjwa huo kwa watoto ambao hukosa raha katika kula na kufanya mambo mengine muhimu.
"Nimefarijika sana kuwa balozi wa Taasisi ya Smile Train Africa na hasa katika kuondoa tatizo la ugonjwa wa mdomo sungura, naomba jamii iunge mkono juhudi za taasisi hii  kwani jukumu letu sisi," alisema.
Taasisi ya Smile Train Afrika hutoa msaada wa kifedha na vifaa ili kusaidia kufidia gharama kwa ajili ya upasuaji. Uwekezaji wote huu si tu kwamba unawezesha upasuaji mkubwa lakini pia unafanya upasuaji huu uwe salama na wenye ubora.

No comments:

Post a Comment