Tuesday, October 24

Marekani na Syria ndizo nchi pekee zimesalia nje ya mkataba wa Paris

A man fishes in Cocibolca Lake in the province of Rivas, about 125km south of the capital Managua, on 4 November, 2013.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNicaragua has been described as a "renewable energy paradise"
Nicaragua imeweka sahihi mkataka wa mabadiliko ya hali ya hewa, ikimaanisha kuwa Marekani na Syria ndizo nchi pekee ambazo hazijaunga mkono mkataba huo.
Mkataba huo unayaleta pamoja mataifa ya dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Nicaragua ilikataa kusaini mkataba huo mwaka uliopita ikisema kuwa haujafikia kiwango cha kutatua tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.,
Mwezi Juni Rais Donald Trump alisema kuwa Marekani itajiondoa kutoka mkataba huo lakini sheria zake zinasema kuwa hilo halitafanyika hadi mwaka 2020.
Rais Trump alisema kuwa ni wajibu wake kuilinda Marekani na ataomba mkataba mpya ambao hautadhuru biashara za Marekani.
Farmer in a Nicaraguan coffee cropHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHighly sought-after Nicaraguan coffee is thought to be particularly susceptible to changes in weather patterns
Wanasayansi wanasema kuwa kazi ya kutekelezwa kwa mkataba wa Paris ni lazima ianze ikiwa kutahitajika kuwa na mafanikio yoyote.
Mkataba huo unajumuisha Marekani na nchi zingine 187 kuweka viwango vya kuongezeka joto dunia chini ya nyuzi joto 2.
Rais wa Nicaragua Daniel Ortega aliashiria wiki iliyipita kuwa angesaini mkataba huo.
"Wanasayansi kutoka chi zilizostawi, wanasayasia wanaofanya kazi na shirika la Nasa, kila mmoja wanakubaliana kuwa ni lazima tusitishe shughuli zinazoharibu sayari ya dunia," alisema Ortega.
Nicaraguan President Daniel Ortega (10 April 2015)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNicaraguan President Daniel Ortega wants tough action to combat global warming
Serikali ya Bw. Ortega awali ilikuwa imesema kuwa mkataba huo haukuwa umeangazia zaidi nchi tajiri kutatua tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.
Rais Trump amedai kuwa mkataba huo, utaathiri Marekani kwa manufaa ya nchi zingine.
Alidai mwezi Juni kuwa mkataba huo utaigharimu Marekani ajira milioni 6.5 na dola trilioni 3 katika pato la taifa.
Hata hivyo hivi karibuni Marekani ilidokeza kuwa ingebadilisha hatua yake ya kujiondoa kutoka mkataba huo.
Tangu jadi Marekani, bara la Ulaya na China wamekuwa wachangiaji wa karibu nusu ya gesi chafu duniani.

No comments:

Post a Comment