Tuesday, October 24

Jeshi la Marekani kuendelea kuhudumu Niger

Mazishi ya sajenti La David Johnson wa Marekani aliyeuawa NigerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMazishi ya sajenti La David Johnson wa Marekani aliyeuawa Niger
Afisa mkuu katika jeshi la Marekani amesema vikosi vya nchi hiyo vitaendelea kutoa usaidizi kwa wanajeshi wa Niger licha ya vifo vya wanajeshi wake wanne.
Wanajeshi hao akiwemo Sajenti La David Johnson, waliuawa katika shambulio la uvamizi.
Mwenyekiti wa wakuu wa wafanyakazi, Jenerali Joseph Dunford, amesema wanajeshi wa kikosi cha kupiga doria usiko hawakutarajia kupata makabiliano na uchunguzi unafanyika kubaininni kilichotokea.
Wiki tatu baada ya shambulio hilo, katika enoe la mashinani Niger, masuali mengi yamesalia kuhusu kilichotokea katika operesheni hiyo ya wanajeshi wa Marekani.
Shambulio hilo liliripotiwa kwanza mnamo Oktoba tarehe 4 kwamba wanajeshi watatu waliokuwa wnapiga doria wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika uvamizi uliotekelezwa karibu na mpaka na Mali.
Inadhaniwa kuwa wapiganaji wa makabila katika eneo hilo wanaohusishwa kushirikiana na Islamic Statendio waliohusika na shambulio hilo.
Kuna wanajeshi 800 wa Marekani wanaotoa usaidizi kwa kikosi kinachoongozwa na Ufaransa kukabilinaa na Islamic State, al-Qaida na Boko Haram Afrika magharibi.

No comments:

Post a Comment