Wednesday, October 25

MAMA SALMA AWAONYA WANAUME WANAOWAAMBIA WANAFUNZI WA KIKE WAMEPENDEZA


Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma amewaonya wanaume kuacha tabia ya kuwaambia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wamependeza kwa lengo la kuwarubuni na kuwashawishi kufanya nao mapenzi.
Rai hiyo amesema hayo mbele ya wahitimu na kidato cha nne katika mahafali ya pili ya Shule ya Sekonadari ya St Marcus iliyopo  Songwe.
Amesema tabia ya kuwasifia watoto wa kike kuwa wamependeza inashamiri  lakini lengo kuu ni kuwashawishi kimapenzi, ni vema tabia hiyo ikakoma na kila mwanajamii inapaswa kuikemea kwa nguzu zote.
“Niwambie wanaume wote wanaowaita wasichana wa shule wamependeza kwa lengo la kuwashawishi kufanya nao mapenzi wakome, waache tena wasiwarubuni watoto kwa maneno hayo machafu ambayo hayafai kwa watoto wa shule.
“Si kosa kwa mwanafunzi wa kike kuwa na rafiki wa kiume kwani ni rafiki wa kiume ambaye anaweza kukusaidia kimasomo lakini si kwa mapenzi. Unapaswa uwe na boyfriend wa kukusaidia kukokotoa Fizikia, bailojia na masomo mengine lakini siyo kufanya mapenzi narudi tena fungeni mapaja yenu’ alisema Salma

No comments:

Post a Comment