Akizungumza leo Alhamisi katika kipindi cha Maisha Mseto kinachorushwa na redio Times FM, Polepole amesema yeye ni muumini wa maoni ya wananchi kwenye mchakato wa Katiba mpya.
Amesema wakati ya mchakato wa Katiba mpya alikuwa miongoni mwa wajumbe waliokusanya maoni ya wananchi ataendelea kuunga mkono maoni yao.
“Nilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima ya Tanzania na ninajua nini Watanzania wanasema kwa hiyo, mimi ni muumini wa maoni ya wananchi,” amesema.
Amesema mchakato huo ulikwama kwa sababu hakukuwepo na uelewa wa nini Watanzania wanataka.
Hata hivyo alidai kuwa mabadiliko makubwa yanayofanywa ndani ya chama hicho yanaakisi kushughulikia kero za wananchi.
“Siasa safi ni kushughulika na kero za wananchi wetu, chama kimejitathmini na kujisahihisha kwa sababu tumepata usahidi kwamba kuna mahali tulikosea kwa hiyo, tunao utaratibu wa kujikosoa,” amesema.
Polepole amesema uongozi wa Rais John Magufuli umejikita zaidi katika kushughulikia kero za wananchi kwa kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uadilifu huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment