Mgogoro kuhusu uhusiano kati ya msanii wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinums na mwanamitindo Hamisa Mobeto umechukua mweleko mpya baada ya Zari Hassan kukana madai ya mpenziwe kwamba alikuwa anajua kwamba alikuwa na uhusiano na mwanamitindo huyo kulingana na gazeti la New Vision Uganda.
Diamond siku ya Jumanne katika mahojiano na Cloud Fm alidai kwamba walitatua tatizo lililopokuwepo kati yake na mama ya watoto wake.
Hatahivyo kulingana na majibu ya Zari katika mtandao mmoja wa kijamii hayo yote yalionekana kuwa uwongo kwa mujibu wa gazeti la The New Vision Uganda.
''Hahaha...unajichezea mwenyewe....uwongo unaozungumza kuhusu mimi kumjua mpenzi wako wa kando ...jaribu kusuluhisha makosa yako na wacha uwongo.
Kunyamaza kwangu hakumaanishi kwamba mimi ni mjinga. Chunguza maneno yako '', Zari aliandika katika mtandao wa Snap Chat.
Aliendelea: Pengine ni kwa sababu mimi ni mama ya watoto wako na ndio maana nimeamua kunyamaza. Tafadhali usinijaribu.
Kulingana na gazeti la New Vision ,alipoulizwa ajibu kuhusu chapisho hilo la Zari , Diamond alisema kwamba anaelewa vizuri kwa sababu kuna vitu ambavyo alifichua katika mahojiano hayo.
Katika mahojiano na idhaa na Cloud Fm nyota huyo alifumbua fumbo la muda mrefu lililokuwa likiwakera mashabiki wake wengi kuhusu uvumi uliokuwa ukisambaa kuhusu uhusiano wake na Hamisa.
Diamond baadaye aliomba radhi kwa Zari Hassan na familia yake.
''Ningependa kuomba radhi kwa mke wangu na watoto kwa makosa hayo'', alisema katika mahojiano.
Bi Mobetto alishiriki katika video ya wimbo wa Diamond Salome ambao umegonga vichwa vya habari .
No comments:
Post a Comment