Wednesday, September 27

Museveni aahidi kukabiliana na mauaji ya wanawake

Yoweri MuseveniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni wa Uganda anasema kuwa atahakikisha usalama unaimarishwa na kuongeza wanausalama na kutoa nyenzo za kisasa kuhusu uchunguzi kufuatia mauaji ya wanawake katika eneo la Entebbe.
Museveni amesema hayo baada ya kutembelea eneo ambako mauaji ya wanawake yamekuwa yakitendeka sehemu za Entebbe.
Rais ameonyesha masikitiko yake na mbinu za sasa zinazotumiwa na polisi kuchunguza mauaji , akisema uchunguzi huo haujazaa matunda yoyote.
Museveni alitembelea kijiji cha Lyamutundwe, Katabi Entebbe na kuzungumza na wananchi huku akiandika katika kitabu chake kile wananchi walichokuwa wanamwambia. Alisikitishwa na mauaji hayo na kusema
"Tutakomesha mauaji haya. Mauaji ni tofauti na vita. Huu ni uhalifu."
Hadi sasa watu 16 wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji ya wanawake hao.
Miili ya wanawake ilipatikana katika eneo hilo ikiwa na vijiti katika sehemu za siri na ikiwa imetupwa msituni pamoja na vichakani katika eneo hilo.
Hadi sasa idadi ya wanawake waliouawa kinyama katika wilaya ya Wakiso mkiwemo Entebbe inafikia 28.

No comments:

Post a Comment