Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amewaachia huru washtakiwa hao leo Alhamisi mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 iliyofabnyiwa marekebisho 2002 na Mahakama kuridhia.
Kishenyi aliomba kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu hicho kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo hakimu aliwaachia huru washtakiwa hao leo saa 4 asubuhi.
Wakati kesi hiyo ikiondolewa mahakamani hapo alikuwapo Lwakatare pekee na mwenzake hakufika kutokana na kuwa matatizo ya kifamilia.
Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Machi 20, 2013.
Katika kesi hiyo walikuwa wakidaiwa kuwa Desemba 28, 2013 katika eneo la King’ong’o, Wilaya ya Kinondoni, kwa pamoja walikula njama za kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Baada ya kuachiwa huru, Lwakatare alimshukuru Mungu kwa kuwa na siku njema na yenye furaha kwake.
No comments:
Post a Comment